Wednesday, July 13, 2011




Washambuliaji wa timu ya taifa ya ZAMBIA na JAMHURI ya KATI kumwaga wino simba

Klabu ya soka ya SIMBA inakamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji FELEX SUNZU wa timu ya taifa ya Zambia na MOMA HILLARIE wa timu ya taifa ya JAMHURI ya KATI ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo ilikuwa butu wakati wa michuano ya kombe ka KAGAME yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na TBC ofisini kwake Afisa Habari wa SIMBA, EZEKEL KAMWAGA amesema SUNZU anatua usiku wa leo kukamilisha usajili wakati HILLARIE ameshafanya majaribio na kikosi cha SIMBA na sasa iliyobaki ni kukamilisha taratibu za usajili.(PAUSE)

KAMWAGA amesema mshambuliaji wa samba EMANNUEL OKWI amefauli majaribio aliyofanya na klabu ya KAIZER CHIEF ya Afrika kusini na sasa anasubiri kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusajiliwa na kama atafeli atarejea kuitumikia SIMBA.

KAMWAGA pia amekanusha uvumi ulionee kwenye vyombo vya habari lakini siyo TBC kwamba kiungo MOHAMED BANKA na mshambuliaji MUSSA MGOSI wametemwa na SIMBA,amesema wachezaji hao ni mali ya SIMBA na watarejea kuitumikia klabu yao baada ya mapunziko mafupi waliyopewa na wawachezaji wengine wa SIMBA baada ya mchezo wa fainali ya kuwania kombe la KAGAME dhidi ya YANGA.

SIMBA itaanza mazoezi wiki ijayo kujiandaa kwa mechi ya ngao ya HISANI dhidi ya YANGA AGOSTI 13 na LIGI KUU ya VODACOM TANZANIA BARA ambayo itaanza kutimua vumbi AGOSTI 20.

====

No comments:

Post a Comment