Monday, July 11, 2011

MEXICO MABINGWA KOMBE LA DUNIA KWA VIJANA



Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya MEXICO imenyakua kombe la dunia kwa vijana baada ya kuichapa URUGUAY kwa mabao MAWILI kwa BILA katika mchezo wa fainali ulichezwa jana katika dimba la ESTADIO AZTECA.

Mabao ya MEXICO yamefungwa na nahodha wao Antonio Briseno na Giovani Casillas na kuifanya MEXICO inyakue ubingwa huo kwa mara ya pili.

Katika mchezo huo wa jana URUGUAY walijaribu kuzawazisha mabao hayo lakini MEXICO wakishangiliwa na mashabiki wao LAKI MOJA katika uwanja wao wa nyumbani wa ESTADIO AZTECA walikaa imaara kulinda lango lao.

MEXICO kwa mara ya mwisho kunyakua ubingwa huo wa dunia kwa vijana wenye umri wa miaka 17 ilikuwa mwaka 2005,NIGERIA ndiyo inayongoza katika orodha ya kunyakua kombe hilo la vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwani wameshatwaa kombe hilo MARA NNE.

===

No comments:

Post a Comment