Monday, July 11, 2011

Marekani yatinga nusu fainali ya kombe la dunia kwa wanawake

Timu ya taifa ya wanawae ya MAREKANI imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake baada ya kuifunga BRAZIL mabao 5-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Timu hizo mbili zilitoka sare ya kufungana magoli MAWILI kwa MAWILI katika dakika 120 za mchezo ndipo ikatumika sheria ya penati ambayo BRAZIL walikosa penati mbili.

Balaa katika timu ya BRAZIL lilianza dakika ya pili ya mchezo huo pale beki wa BRAZIL DIANE alipojifunga mwenyewe wakati akiwa katika juhudi za kutaka kuondoa mpira kwenye hatari.

BRAZIL ilizawazisha bao hilo katika dakika ya 68 kupitia kwa mchezaji bora wa dunia kwa wanawake MARTA kwa njia ya mkwaju wa penati.

Katika muda wa dakika za nyongeza MARTA tena akaipatia BRAZIL bao la pili kwenye dakika ya 93 lakini MAREKANI walisawazisha bao hilo zikiwa zimesalia sekunde chache mpira kumalizika ABBY WAMBACH akiipatia bao la pili MAREKANI kwa kichwa na kufanya mchezo huo kuamuliwa kwa njia ya penati.

DIANE alikwenda kupiga penati ili afute makosa yake ya kujifunga lakini mambo yakazidi kuwa mabaya kwake kwani penati yake ilipanguliwa na kipa wa MAREKANI SOLO huku MAREKANI wakipata penati yao ya mwisho na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya kombe hilo na UFARANSA siku ya JUMATANO.

Nusu fainali nyingine itakua kati ya JAPAN NA SWEDEN.

= = = = = =


No comments:

Post a Comment