Monday, July 18, 2011

ZANZIBAR YAnyakua dhabu NNE katika JUDO

ZANZIBAR YAnyakua dhabu NNE katika JUDO

TIMU ya taifa ya JUDO ya ZANZIBAR inaongoza baada ya kujinyakulia medali NNE za dhahabu katika mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika MASHARIKI yanayoendelea jijini DSM.

Akizungumza na TBC kwa njia ya simu katibu mkuu wa chama cha JUDO TANZANIA KASHINDE SHABANI amesema BURUNDI na KENYA zinashika nafasi ya pili zikiwa na medali mbili za dhahabu kila moja.

SHABANI amesema timu ya JUDO ya Tanzania bara mpaka sasa imejinyakulia medali mbili za SHABA.

Mashindano hayo yanashirikisha nchi za KENYA, BURUNDI, ZANZIBAR na wenyeji TANZANIA BARA.

====
Mabondia chipukizi watambiana katika masubwi

Katika masubwi bondia chipukizi JULIAS THOMAS wa klabu ya MIDIZINI ameibuka kidedea baada ya kumchapa MARK HARDSON wa klabu ya Ashanti katika uzito mwepesi wa KILO 52 kwenye mashindano ya kuinua vipaji kwa mabondia jipukizi yaliyofanyika jana jijini DSM.

Pambano jingine la kusisimua liliwakutanisha JONAS LAZARO wa klabu ya MAGOMENI CITY dhidi ya MOHMED SEIF na katika pambano hilo JONAS alimpinga SEIF kwa POINTI.

Mabondia wenye umri chini ya miaka 12 iliwakutanisha JAMES EDMOND wa MIDIZINI dhidi ya STEVIN ANASTARS pia wa midizini katika uzito wa kilo 31 na katika pambano hilo walitoka sare.

Kwa upande wa akina dada ZAINABU MHANULA alicheza na ZULFA SADIKI katika uzito wa kilo 31 na pia wakatoka sare.

===

Japan mabingwa wa kombe la dunuia kwa wanawake

Timu ya taifa ya wanawake ya JAPAN imenyakua kombe la dunia kwa wanawake baada ya kuifunga MAREKANI kwa mikwaju ya penati MITATU kwa Moja baada muda wa dakika 120 kushuhudia timu hizo sikitoka sare ya kufunga mabao MAWILI kwa MAWILI.

ABBY WAMBACH aliifungia MAREKANI bao la pili katika dakika za nyongeza lakini nahodha wa JAPAN HOMARE SAWA akasawazisha bao hilo kwa JAPAN katika dakika ya 117 na mchezo kuimalizika kwa kufungana mabao MAWILI kwa MAWILI baada ya dakika 120 za mchezo kumalizaika.

Goli la kuongoza la mareikani limefungwa na ALEX MORGAN na JAPAN wakasawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Aya Miyama katika dakika ya 81 ya mchezo.

Katika hatua ya penati,MLINDA wa MLANGO wa JAPAN Ayumi Kaihori aliibuka shujaa baaada ya kuokoa penati mbili za MAREKANI.

JAPAN katika mikwaju ya penati ikapata penati TATU na MAREKANI penati moja hivyo JAPAN wakakabidhiwa kombe la ubingwa wa dunia kwa wanawake.


= = = = =

Paraguay yaitupa nje Brazil Copa America

Timu ya taifa ya Paraguay, imetinga hatua ya NUSU FAINALI ya COPA AMERIKA baada ya kuitandika mabingwa watetezi BRAZIL kwa mikwaju ya penati 2 kwa BILA.

BRAZIL walitwala kipindi chote cha dakika 120 za mchezo huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake wakiongozwa na PATO, Robinho na Neymar wakishindwa kuzitumi vyema na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana.

Katika hatua ya kupigiana penati maajabu yakatokea baada ya wachezaji watano wa Brazil kukosa penati zao,penati nne wakipinga nje ya lago,wakati penati moja ilidakwa na kipa wa Paraguay Justo Villar.

Waliokosa penati kwa upande wa BRAZIL ni Elano, Andres Santos na Thiago Silva huku penati za PARAGUAY zikifungwa na Marcelo Estigarribia na Cristian Riveros.

Katika mchezo mwingine wa Robo Fainali ulishudia VENEZUELA ikiitandika CHILLE kwa mabao MAWILI kwa MOJA.

Hatua ya NUSU fainali itakayochezwa kesho kutwa itazikutanisha PERU na URUGUAY na PARAGUAY dhidi ya VENEZUELA.

==== ===

Daniel Pedrosa ashinda Germany Moto GP

Daniel Pedrosa ameshinda mbio za pikipiki za Germany Moto GP baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika 41 na sekunde 12.

Katika mbio hizo za UJERUMANI Jorge Lorenzo ameamaliza katika nasafi ya pili wakati nafasi ya tatu imenyakuliwa na bingwa wa dunia Casey Stoner,Andrea Dovizioso na Ben Spies wameamaliza katika nafasi ya nne na ya tano.

Msimamo wa jumla unaonyesha Casey Stoner anaongoza akiwa na Alama 168, Jorge Lorenzo anashika nafasi ya pili akiwa na alama 153 ,Andrea Dovizioso yupo katika nafasi ya tatu akiwa na alama 132 ,Valentino Rossi ni wane akiwa na alama 98 na Daniel Pedrosa anashika nafasi ya tano akiwa na alama 94.

===== ===


MARK CAVENDISH ashinda mbio za baiskeli za UFARANSA.

Katika mbio za baiskeli za Ufaransa, MARK CAVENDISH imeibuka kidedea baada ya kushinda hatua ya 15 mbio hizo jana.

Katika mbio hizo TYLER FARRAR imeshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikatwaliwa na ALESSANDRO PETACCHI.

Matoke ya jumla baada ya hatua hizo kumi na tano THOMAS VOECKLER anaongoza akifutiwa na FRANK SCHLECH na watatu ni CADEL EVANS.

Hatua ya kumi na sita ya mbio za baiskeli za UFARANSA yataendelea leo.


===== ====

No comments:

Post a Comment