Monday, July 4, 2011

ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME KESHO

Mabingwa mara sita wa kome la KAGEME timu ya SIMBA kesho inashuka dimbani kuikabili BUNAMWAYA ya UGANDA katika mchezo wa robo fainali ya pili itakayopigwa katika uwanja wa taifa.

Robo fainali ya kwanza itakayochezwa majira ya saa nane mchana itazikutanisha mabingwa wa Kenya, ULINZI itakayoteremka dimbani dhidi ya EL- MEREIKH ya SUDAN.

Wakata Simba ikikabili BUNAMWAYA watani wao wa jadi YANGA waliomaliza vinara katika kundi la B itacheza na READ SEA ya ERITREA siku ya jumatano.

Mechi nyingine ya robo fainali ya siku ya jumatano ambayo itachezwa saa nane mchana itazikutanisha mabingwa wa ETHIOPIA ST.GEORGE dhidi ya VITAL O ya BURUNDI.

Katika michezo iliyopigwa jana kwenye uwanja wa taifa jijini DSM SIMBA ililazimishwa kutoka sare ya bila kufungana na READ SEA ya ERITREA.

Katika mchezo uliochezwa mapema ZANZIBAR OCEAN VIEW wameondolewa katika mashindano hayo na VITAL ‘O baada ya kufungwa bao MOJA kwa BILA.

===

URUGUAY YATINGA NUSU FAINALI U-17

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya URUGUAY imetinga katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya konmbe la dunia kwa vijana baada ya kuifunga UZBEKISTAN mabao MAWILI kwa BILA.

Mabao mawili ya URUGUAY yamepachikwa wavuni na SANTIAGO CHARAMONI na RODRIGO AGUIRRE.

Leo kutakuwa na mchezo mwingine wa kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali wakati UJERUMANI itakaposhuka dimbani kuikabili ENGLAND.

Kesho utachezwa mchezo mmoja wa robo fainali wakati UFARANSA itakapoikabili MEXICO.

===

BRAZILI YASHINDWA KUTAMBA COPA AMERICA

Mabingwa watetezi wa kombe la COPA AMERICA timu ya taifa ya BRAZIL imeanza vibaya kutetea ubingwa huo babada ya jana kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na timu ya taifa ya VENEZUELA.

BRAZIL ilicheza kwa uolewano mkubwa na kumiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo lakini washambuliaji wake wakiongozwa na PATO ROBINHO na NEYMAR walishindwa kuvifumani nyavu za timu ya taifa ya VENEZUELA.

Mchezo mwingine ulizikutanisha PARAGUAY na ECUADOR ambao nao wametoka sare ya bila kufungana.

Michuno hiyo ya kuwania kombe la COPA AMARIKA inaendelea kesho kwa michezo miwili kuchezwa, URUGUAY itaikabili PERU huku CHILE ikiteremka dimbani dhidi ya MEXICO

= === = = ===

BARAZIL yatinga robo fainali ya kobe la DUNIA kwa wanawake

Timu ya taifa ya wanawake ya BARAZIL imetinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia kwa wanawake baada ya kuichapa NORWAY mabao MATATU kwa BILA.

Brazili ikiongozwa na mchezaji bora wa dunia kwa wanawake MARTA walijipatia bao la kuongoza lilokwamishwa wavuni na MARTA mwenyewe baada ya kuwapiga chenga walizi kazaa wa NORWAY.

ROSANA akawanyanyua kutoka vitini mashabiki wa BRAZIL baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya 46 ya mchezo safari hii kwa shuti kali lilokwenda moja kwa moja wavuni akimalizia pasi nzuri ya MARTA

Msumari wa mwisho katika jeneza la NORWAY ulipigiliwa na MARTA katika dakika ya 48 alipoifungia BRAZIL bao la 3 likiwa ni bao lake la pili katika mchezo huo wa jana.

Katika mchezo mwingine wa kombe hilo AUSTRALIA imeifunga wawakilishi wengine wa Afrika timu ya taifa ya EQUATORIAL GUINEA mabao MATATU kwa MAWILI.

= = = = = == =

NOVAK DJOKOVIC bingwa WIMBLEDON

NOVAK DJOKOVIC ndiye mchezaji namba moja kwa ubora wa tenesi duniani baada ya kumchapa RAFAEL NADAL aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo katika mchezo wa fainali wa michuano ya WIMBLEDON iliyofanyika jana.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa DJOKOVIC kunyakua taji hilo la WIMBLEDON.

Katika mchezo wa jana DJOKOVIC amemfunga NADAL kwa seti tatu kwa moja kwa ushindi wa 6-4 6-1 1-6 6-3.

Katika viwango vya ubora wa tenesi dunia ambayo vimetolea leo hii na shirikisho la tenesi dunia Novak Djokovic anashika namba moja akiwa na ALAMA 285, NADAL anaporoka hadi katika nafasi ya pili akiwa na ALAMA 270, ROGER FEDERER inashika nafasi ya tatu akiwa na ALAMA 230, ANDY MURRAY ni wa nne akiwa na Alama 206 na ROBIN SODERLING anashikilia nafasi ya tano.

= = = = = = =

Evans ASHINDA MBIO ZA BAISKELI ZA UFARANSA

Mwedesha baiskeli wa timu inayovalia jezi za rangi ya njano CADEL EVANS ameshinda hatua ya pili ya mbio za baiskeli za UFARANSA zilizokuwa na ubali wa KM 23.

Katika mbio hizo za jana mwedesha baiskeli mwezake wa timu ya jezi ya njano ANDY SCHLECK alimaliza katika nafasi ya pili.

Bingwa mtetezi wa mbio hizo ALBERTO CONTADOR alimaliza katika nafasi ya tatu akiwa nyuma kwa muda wa dakika MOJA na sekunde kumi na saba wakati Evans na Schleck wakiongoza kwa muda wa dakika moja na sekunde KUMI NA NNE.

Hatua ya tatu ya mashidano hayo yataendelea leo nchini UFARANSA.

===

No comments:

Post a Comment