Tuesday, July 12, 2011

u-23


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23, JAMHURI KIHWELO amewita katika kikosi cha wachezaji 20 GEORGE MTEMAHANJI anayekipinga katika timu ya Modeva FC, Italia kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya SHELISHELI,michezo itakayopingwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha july 27 na 30.

Akitangaza kikosi hiyo jijini DSM hii leo kocha KIHWELO amesema amemuongeza mchezaji huyo anayesukuma ngozi nchini ITALIA ili kuimarisha kikosi chake na kubainisha kuwa michezo hiyo miwili itasaidia kuwapa wachezaji uzoefu ya michezo ya kimataifa.(PAUSE)


KIHWELO akatangaza majina ya wachezaji wengine aliowaita katika kikosi cha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 kuwa ni Juma Abdul (Mtibwa Sugar), Himid Mao (Azam), Babu Ally (Morani), Shabani Kado (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam), Seif Juma (Ilala), Khamis Mcha (Azam), Shomari Kapombe
(Simba), Jackson Wandwi (Azam).

Wengine ni Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Thomas Ulimwengu (Humbarg SV, Ujerumani), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Mohamed Soud (Toto Africans), Jamal Mnyate (Azam), Awadh Juma (Moro United), Salum Kanoni (Simba), Salum Telela (Yanga), Samuel Ngasa (African Lyon) na George Mtemahanji (Modeva FC, Italia).

U-23 wataanza mozezi july 18 katika uwanja wa karume na wataondoka kwenda arusha JULY ishirini wakati wapinzani wao timu ya taifa ya SHELISHELI itawasili nchini JULY 21


No comments:

Post a Comment