Tuesday, July 12, 2011

YANGA KUFURAHIA KOMBE


Klabu ya soka ya YANGA imekanusha habari zilioandikwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kumuuza beki wake wa kutumainiwa NADIR HAROUB ALI katika klabu ya soka ya EL MERREIKH ya SUDAN.

Katibu Mkuu wa YANGA CELESTIN MWESIGWA amesema hakuna makubaliano yoyote ama maombi kutoka EL MERREIKH juu ya kumuhitaji beki huyo na pia amesema YANGA iko tayari kukamilisha malipo ya usajili wa mchezaji OSCAR JOSHUA kutoka RUVU SHOOTING.(PAUSE)

Amesema TATIZO lililotokea ni uongozi wa RUVU kujipanga na kuhakikisha unapata malipo ya usajili wa mchezaji huyo ambapo awali yalijitokeza makundi mawili yakitaka kulipwa kwa fedha taslimu gharama za uhamisho wa mchezaji huyo.


No comments:

Post a Comment