Wednesday, July 21, 2010

VIFAA SIMBA


Simba na Yanga zapewa vifaa tayari kwa ligi kuu Tanzania bara.
Watani wa jadi katika soka la Tanzania Simba na Yanga leo wamekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 64 na wadhamini wao kampuni ya bia ya TBL tayari kwa mikiki mikiki ya ligi kuu Tanzania bara ambayo inaanza kutimu vumbi kuanzia AGUST 21.
Maneje wa bia ya Kilimanjaro GEORGE KAVISHE amesema wametoa vifaa hivyo kama mkataba wao na vilabu hivyo unavyosema
Kwa upandea wao mkamu mwenyekiti wa SIMBA GEOFREY NYANGE maarufu kama KAMBURU na mwenyekiti wa YANGA LLOYD NCHUNGA wamesema vifaa hivyo watavitumia kwa ajili ya kuendeleza soka la Tanzania. (VOX POPS)Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wao wanateremka dimbani kuivaa African Lyon nyumbani kwenye dimba la UHURU jijini DSM wakati watani wao YANGA watasafiri hadi DODOMA kupepetana na POLISI DODOMA katika dimba la Jamhuri

No comments:

Post a Comment