Monday, July 26, 2010

NGORONGORO HEROES yafungwa Ivory Coast


Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 NGORONGORO HEROES imeanza vibaya mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana baada ya hiyo jana kuzabwa bao moja kwa bila na timu ya taifa ya vijana ya IVORY COAST mjini ABJAN.
NGORONGORO HEROES itabidi ifanye kazi ya ziada kuhakikisha inapata ushindi nyumbani kama inataka kusonga mbele katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika nchini LIBYA mwakani.Mchezo wa marundiano utachezwa baada ya wiki mbili zijazo jijini DSM

No comments:

Post a Comment