Tuesday, July 27, 2010

Netball


Kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mashindano makubwa baadhi ya wachezaji wa timu za NETBALL zinazoshiriki mashindano ya klabu bingwa ya TAIFA wameanza kukata tamaa kwa timu zao kutwa ubingwa.

Wachezaji hao ROSE ISRAE wa EMIMA ambayo imeshapoteza michezo yote iliyocheza anasema uzoefu umewaangusha huku JAMILA ISSA wa RAS LINDI akisema timu za mikoani hazina uzoefu wa kutosha wa kutwa ubingwa huo.

Baadhi ya michezo iliyochezwa leo asubuhi timu ya RAS LINDI imeilaza SIFA kwa mabao 35 kwa 12,FBS ikapokea kipigo cha mabao 25 kwa 17 toka kwa MAGEREZA,JESHI STARS imeifunga POLISI DAR ES SALAAM kwa mabao 24 kwa 18 huku TUMBAKU MOROROGO ikiifunga EMIMA magoli 44 kwa 14.
Katika michezo mingine MAPINDUZI imefungwa na POLISI MBEYA kwa mabao 18 kwa 14 na timu ya MAGANGA haikutokea uwanjani kucheza na POLISI MWANZA kwamaana hiyo POLISI MWANZA wamepata ushindi wa mezani wa mabao 40 kwa bila.

Michezo hiyo ya klabu bingwa ya Netball inafanyika katika viwanja vya TCC CHANG’OMBE jijini DSM

No comments:

Post a Comment