Wednesday, July 21, 2010

NGORONGORO HEROES YAANGWA


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama ngorongoro heroes inaendela na kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la mataifa ya AFRIKA na inashuka dimbani dhidi ya IVORY COAST siku ya jumapili kwenye dimba la FELEX HOUPHOUET BOIGNY mjini ABJAN.
Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa NGORONGORO HEROES mkurungezi wa michezo katika wizara ya habari utamaduni na michezo LEORNARD THADEO amewataka vijana hao kucheza kwa bidii na nidhamu ya hali juu ili kushinda mchezo huo ugenini na kufanya kazi iwe rahisi wataporundiana jijini DSM wiki baada ya wiki mbili zijazo.
Kocha mkuu wa NGORONGORO HEROES, RODRIGO STROCKELER na nahodha wa timu hiyo HIMID MAO wamesema wao ni jeshi la uhakika na wemejiandaa vyema kushinda mchezo huo.
Msafara wa wachezaji 20 na viongozi saba NGORONGORO HEROES unaondoka alfajiri ya kesho tayari kuikabili timu ya taifa ya vijana ya IVORY COAST siku ya jumapili.NGORONGORO HEROES iwapo itashinda mchezo huo itakutana na mshindi kati ya timu ya taifa ya vijana ya NGAMBIA ambayo inateremka dimbani kuivaa SERE LEONE,fainali za AFRIKA kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 zitafanyika nchni LIBYA mwakani

No comments:

Post a Comment