Tuesday, July 27, 2010

Kozi ya uongozi katika michezo


Washiriki wa semina ya uongozi katika michezo wamesema mafunzo wanayoyapata yataleta mapinduzi katika maendeleo ya michezo hapa nchini.
RAIS wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT, JOAN MINJA na kocha wa mchezo wa tenisi BOAZI MWAKUSA wamesema wamejifunza mambo mbalimbali ya kiongozi katika michezo kama vile kuandaa mpango mkakati wa maendeleo wa muda mfupi na muda mrefu ambao awali walikua hawajui njisi ya kufanya hivyo.

Semina hiyo ya uongozi katika michezo inaendeshwa na kamati ya Olympiki Tanzania kwa ushirikiano na OLYMPIC SOLIDARITY ikiwa na lengo la kuwapiga msasa viongozi wa vyama vya michezo Tanzania na inafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini DSM.

No comments:

Post a Comment