Monday, July 19, 2010

Uchaguzi Yanga


LLYORD CHUNGA ndiye mwnyekiti mpya wa YANGA baada ya kushinda Uchanguzi.
Mwasheria LLYORD CHUNGA ndiye mwenyekiti mpya wa klabu ya YANGA baada hiyo jana kuchanguliwa na wanachama wa YANGA katika uchanguzi uliofanyika katika ukumbi wa PTA sasaba jijini DSM
Afisa habari wa YANGA LUIS SEDEU amesema CHUNGA ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia kura 1437 baada ya kuwabwanga washindani wake EDIGAR CHIBULA, FRANCIS KIFUKWE, ABEDI ABEDI na MBARAKA IGANGULA.
SEDEU amesema DAVIS MOSHA amechanguliwa kama makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 2142 na kumshinda mpinzania wake COSTANTINTINE MALIGO aliyejinyakulia kura 55
Katika nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji SEDEU amewataja walichanguliwa kuwa ni mchezaji wa zamani wa YANGA na Taifa Stars ALLY MAYAYI,SARA RAMADHANI,MOHAMED BINDA,CHARLES MGONDO,SALUM RUPIA,TITO OSORO TINESI RUTASHABORWA na mwimbaji maarufu wa taarabu nchini MZEE YUSUFU
Viongozi waliochanguliwa wanachukua nafasi ya uongozi wa YANGA uliomalizia muda wake ambao ulikuwa chini ya mwenyekiti IMAN MADEGA.
=

No comments:

Post a Comment