Tuesday, September 28, 2010

AMERIKANI FOOTBALL TANZANIA



Tanzania kwa mara ya kwanza itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa AMERICAN FOOTBALL kati ya DRAKE UNIVERSITY ya MAREKANI dhidi ya CANADEIP ALL STARS ya MEXICO mchezo utakochezwa mjini MOSHI MAI 21 mwakani.
Akizungumza na TBC jijini DSM mratibu wa mchezo huo mwenyekiti wa GLOBALL FOOTBALL PATRICK STEENBERGE kutoka MAREKANI amesema lego la mchezo huo ni kueneza mchezo huo hapa nchini pamoja na kujifunza tamaduni mbalimbali za kitanzania.
Kwa upande wake kaimu Afisa masoko Mkuu wa bodi ya utalii Tanzania DEVOTE MDACHI amesema mchezo huo utasasaidi kuutangaza utalii wa Tanzania kimataifa.
Wachezji wa timu hizo mbili za DRAKE UNIVERSITY ya MAREKANI na CANADEIP ALL STARS licha ya mchezo huo pia wataendesha kliniki za mcezo huo kwa watoto wa shule za sekondari na msingi mkoani Kilimanjaro kabla ya kupanda mlima kilimanjaro

No comments:

Post a Comment