Tuesday, September 28, 2010

TFF yaonyesha makali yake

Rungu la kamati ya mashindano ya shirikisho la soka nchini TFF limewashukia waamuzi wanne wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuwafungia kwa kipindi cha miezi sita kuchezesha michezo ya ligi hiyo baada ya kushindwa kutafsiri sheria 17 za soka katika michezo kazaa iliyopita.
Akizungumza na waadishi habari jijini DSM hii leo Afisa habari wa TFF, FOLRIAN KAIJAGE, aliwataja wamuzi walifungiwa kuwa ni METHEW AKRAMA na FRANK KOMBA waliochezesha mchezo kati ya mabingwa watetezi Simba dhidi ya AZAM FC mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga septemba 11 na Simba kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja
KAIJAGE pia akawataja wamuzi wengine waliofungiwa na kamati hiyo kuwa ni RONALD SWAI na Msaidizi wake SAMUEL PENZU waliochezesha mchezo kati ya YANGA na KAGERA SUKARI kwenye uwanja wa JAMHURI MKOANI MOROGORO na wamuzi hao kushindwa kutafrisi kwa usahihi sheria za soka na kuasababisha YANGA kufunga bao la kwanza,katika mchezo huo YANGA ilipata ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA
KAIJAGE akayataja maamuzi mengie ambayo yamefikiwa na kamati ya mashindano kuwa ni kuipiga faini klabu ya majimaji ya Songea ya shilingi LAKI TATU kwa kile alichoeleza kuwa majimaji ilichelewa kuingia uwanjani kwa dakika 15 na kusababisha mchezo huo kati yake na AFRICAN LYON kuchelewa kuanza,Majimaji wamedaiwa kuchelewa kuingia uwanjani kutokana na imani za kishirikiana katika mchezo ulipigwa kwenye uwanja wa majimaji SEPTEMBA 28.KAIJAGE amesema kamisaa wa mchezo kati ya YANGA na KAGERA SUKARI yeye amefungiwa kwa mwaka mmoja kwa kushindwa kuandika taarifa sasahihi za mchezo huo

No comments:

Post a Comment