Wednesday, September 15, 2010

Makocha waendelea na kozi ya FIBA


Makocha wa mchezo wa mpira wa kikapu wanaohudhuria mafunzo ya siku kumi katika viwanja vya DON BOSCO jijini DSM wamatakiwa kupambana na changamoto mbalimbali zinazoukabili mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkufunzi kutoka shirikisho la kimataifa ya mpira wa Kikapu FIBA SAMWELI WANJOHI raia wa Kenya alilizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa vifaa,muda,wadhamini,tofauti ya vipaji kwa vijana,fedha na hali ya hewa.

WANJOHI amewataka makocha hao kupambana na changamoto hizo kama wanataka kuhakikisha mchezo huo unasonga mbele na kufika katika kiwango cha kimataifa.

Kozi hiyo inashishikisha makocha 20 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchni na inaendeshwa na shirikisho la mpira wa kikapu hapa nchini TBF na lile la kimataifa FIBA.


No comments:

Post a Comment