Tuesday, September 21, 2010

MBIO ZA MAGARI


Tamasha kubwa la magari maarufu kama TANZANIA AUTOMOTIVE FESTIVAL linatarajia kufanyika OCTOBA 1-3 mwaka huu jijini DSM katika viwanja vya Posta.

Mratibu wa Tamasha hilo ALLY MTAAGA amesema hiyo inakuwa ni fursa ya kuhamasisha michezo ya mbio za magari inayokuwa kwa kasi hapa nchini na siku hiyo pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya kuchezea magari na pikipiki .

Tamasha hilo linaloshirikisha wadau wa fani ya magari kutoka nchi mbalimbali Duniani, linadhaminiwa na makampuni ya SUPERDOL, SYNOVATE, AUDIO SENNSATION, INOCH na PETER GEORGE GARAGE pia litatoa fursa kwa watazamani kujionea aina mbalimmbali za magari ya kifahari , yale ya kale na yenye kasi kubwa yanayotumika katika mbio za magari za kimataifa.


No comments:

Post a Comment