Wednesday, September 15, 2010

BMT yawa mbogo kwa SHIMISEMITA


Baraza la Michezo la taifa latangaza kamati ya muda ya shirikisho la michezo la wafanyakazi wa serikali za miataa tanzania SHIMISEMITA ambalo litafanya kazi kwa muda wa siku tisini kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa kudumu.

Akitangaza kamati hiyo mbele ya waandishi Habari,Afisa wa BMT, MOHMED KIGANJA, amesema wamefikia uamuzi wa kutangaza ungozi huo wa muda kutokana na kulega lega kwa uongozi uliokuwepo madarakani.

KIGANJA, aliwataja walioteuliwa na BMT kuunda kamati hiyo ya muda ya SHIMISEMITA kuwa ni Mwenyekiti Stephene Ditenya,makamu mwenyekiti Cloud Mpelembwa huku katibu akiwa ni Salehe Lubawa.

Kiganja aliwataja wajumbe wengine wa SHIMISEMITA kuwa ni Jumanne Mrimmy,Dinnaha Mhomba,Salimu Sanga,Iman Kasagala,Omega Shuma na Amosi Chiwaya.

Kiganja amewataka viongozi hao kuhakisha wanarekibisha katiba ya chama hicho,kufanya uchaguzi na kufanya kazi za kila siku za shirikisho hilo katika kipindi cha siku tisini walizopewa.


No comments:

Post a Comment