Tuesday, September 21, 2010

Ngumi


Maandalizi ya mapambano ya kukata na shoka ya mchezo wa NGUMI na ule wa NGUMI na Mateke maarufu kama KICK BOXING ya bingwa wa mabingwa yanaendelea huku mabondia wote wakijifua kwa ajili ya kupanda ulingoni Octoba 2.

Mratibu wa mapambano hayo ambaye pia ni mwalimu wa mabondia hao JASETH KASEBA amesema mabondia watakaofanya vema wataunda kikosi kitakachoiwakilisha Tanzania Katika mashindano ya Afrika yatakayotimua vumbi nchini KENYA mwezi ujao .

Mapambano hayo yanavuta hisia za wapenda masumbwi kufuatia kuwahusisha mabondia wenye majina makubwa hapa nchini akiwemo bingwa wa Tanzania wa TPBO NA TPBC KARAMA NYIRAWIRA ambaye nia yake kubwa ni kurejesha heshima ya mchezo huo na atapanda ulingoni katika ukumbi wa ILALA AMANA dhidi ya STANLEY KESSY.


Unaweza kudhani kwa vile mchezo wa masumbwi ni wa kutumia nguvu na hatari hivyo ni vigumu kwa wanawake na watoto kushiriki lakini hapa mwanadada UPENDO NJAU na kijana MBARAKA KHATIBU wanatoa shaka juu la hilo


Takribani mabondia thelethini wa NGUMI na zile za MATEKE KICK BOXING watarushiana masumbwi kwa muda wa siku mbili ili kuwapata mabingwa wa mabingwa katika michezo itakayopigwa kwenye ukumbi wa ILALA AMANA jijini DSM mwezi ujao.


No comments:

Post a Comment