Monday, September 27, 2010

squish dar yarindima


BRUCE CHIKABUKA ameibuka kidedea katika mashindano ya ya BELL SQUISH ambayo yamefika tamati hiyo jana katika viwanja vya GYHKHANA jijin DSM baada ya kumfunga ALLY REMTULLA kwa Alama 27 kwa 16.

Kwa upande wa akina dada, VICKY CHUWA emanyakua ubingwa baada ya kumchapa mpinzania wake SARAH EMERSON kwa Alama 32 kwa 10

Nahodha wa KLABU ya GYHKHANA MARWA BUSIGARA amesema igawa mashindano ya mwezi huo yamekua na ushindani mkubwa lakini amesikitishwa na uchache wa ushiriki wa akina DADA

Kwa upande wao wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya DEAUTO GROUP kupitia kwa SIBTAIN REMTULLA wamesema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji vya kucheza Squish lakini wanakosa kuendelezwa ili wacheze katika kiwango cha kimataifa.

Zaidi ya wachezaji AROBAINI wameshiriki katika mashindano hayo kutoka katika mikoa ya ARUSHA, TANGA,DSM na ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment