Monday, September 27, 2010

Michezo leo

Yanga emeengelea kujikita kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya hiyo jana kuibuka na ushinda wa mabao MAWILI kwa BILA dhidi ya RUVU SHOOTING STARS mchezo uliochezwa katika uwanja wa JAMHURI mkoani morogoro.

Kwa matokeo hayo YANGA imefikisha Alama 16 baada ya kushuka dimbani mara SITA ikifuatiwa na mabingwa watetezi SIMBA yenye Alama 12 baada ya kucheza michezo MITANO huku JKT RUVU ikishika nafasi ya tatu ikiwa na Alama 10.

Timu zilizopanda daraja msimu huu bado hazijafanya vyema na zinaendelea kushikilia nafasi za mwisho katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, RUVU SHOOTING inashika nafasi ya 11 ikiwa na Alama 3 baada ya kushuka dimbani mara TANO wakati AFC ARUSHA inaendelea kushikilia mkia ikiwa na haina hata Alama yeyote baada ya kushuka dimbani mara nne na kupoteza michezo yote.

Ligi hiyo inaendelea jumatano ya wiki hii wakati mabingwa watetezi SIMBA watakuwa wageni wa MTIBWA SUKARI kwenye dimba la JAMHURI mjini morogoro,Azam fc watakuwa wenyeji wa JKT RUVU katika dimba la mkwakwani mkoani Tanga.

=== ==

MICHAEL OWEN alifunga goli lake la 200 katika ligi kuu ya ENGALAND na kuisaidia MANCHESTER UNITED kutoka sare ya kufungana mabao MAWILI kwa MAWILI na BOLTON ugenini katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja REEBOK hiyo jana.

Kocha wa MANCHESTER UNITED SIR ALEX FERGUSON amesema ni vizuri kufunga mabao lakini haifurahishi kuona timu inashindwa kuondoka na Alama zote tatu.

Alipoulizwa juu ya timu yake kushindwa kuyatumia matokeo ya jumamosi ya kufungwa kwa wapinzani wao katika kufukuzia ubigwa ARSENALna CHELSE, FERGUSON amesema timu hupoteza Alama wakati hukutegemea matokeo yagekuwa hivyo.

Kwa sare hiyo Manchester imechupa hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya ENGLAND ikiwa na Alama 12 huku ARSENAL wakiendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na Alama 11 baada ya juzi kuchapwa kwa mabao tatu kwa mawili na WEST BROM, kuku mabingwa watetezi CHELSEA wakibaki kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na ALAMA 15 igawa ilichapwa bao moja kwa bila ma MANCHESTER CITY mwishoni mwa wiki.

Kocha mpya wa ASTON VILLA GERARD HOULLIER akiwa kwenye benchi la timu hiyo kwa mara ya kwanza aliingoza VILLA kuibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa Moja dhidi ya BLACKBURN ROVERS.

Matokeo mengine yakushangazwa hiyo jana yameshuhudia NEW CASTLE wakichapwa nyumbani katika uwanja wa ST JAMES PARK kwa mabo mawili kwa moja na STOKE CITY.

=== ==

Ligi kuu ya Hispania maarufu kama LALIGA iliendelea mwsihoni mwa wiki huku BARCELONA wakibuka kidea kwa ushi wa mabo matutu kwa moja dhidi ya ATHLETIC BILIBAO.

VALENCIA nayo ikaibuka na ushindi wa mabao mwawili kwa bila dhidi ya Sporting gijon,SEVILLA ikachapwa mabao 2 kwa bila na HERCULES huku DEPOTTIVO LA CORUNA ikiifungwa na ALMERIA kwa mabao 2-0.

Real Madrid wakabanwa bavu na LAVENTE na kutoka suluhu,real sociedad ikafungwa na MALLORCA kwa maabao mawili kwa sifuri,matokeo mengine ESPAANYOL ikapata ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Osasuna.

Msimamo wa ligi unaonyesha,VALENCIA wanaogoza ligi hiyo wakiwa na Alama 13 na inafuatiwa na mabingwa watetezi BARCELONA wakiwa na Alama 12 real Madrid wanashika nafasi ya tatu wakiwa na Alama 11

== ==

Mkenya PATRICK MAKAU ashinda BERLIN MARATHON

Mkenya PATRICK MAKAU ashinda BERLIN MARATHON ameshinda mashindano ya marathon ya Berlin lakini akashindwa kuvunja rekondi ya mwiethiopia GEBERSELASSLES aliyoweka mwaka 2008.

Makau amemaliza mbio hizo kwa muda wa dakika moja zaidi ya rekondi inayoshikiliwa na GEBERSELASSLES kwani alitumia muda wa saa mbili,dakika TANO na sekunde 8 huku MKENYA mwezake GEOFFREY MUTAI akimaliza katika nafasi ya pili kwa sekunde mbili nyuma ya MAKAU.

Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na mwiethiopia BAZU WORK baada ya kutumia muda wa saa mbili,dakika tano na sekunde 25.

Kwa upande wa wanawake ABERU KEBEDE wa ETHIOPIA amemaliza wa kwanza mbele ya BEZUNESH BEKELE kwa muda wa masaa 2 na dakika 23 na sekunde 58.

== ===

Katika mbio za magari mwendesha magari wa timu ya FERRARI FERNANDO ALONSO ameibuka kideda baada ya kushinga mashindano ya SINGAPORE GRAND PRIX hiyo jana na kuufanya ubingwa wa dunia uwe wazi na unaweza kunyakuliwa na dereva yeyote.

SEBASTIAN vettel akamaliza katika nafasi ya pili nafasi ya tatu ikamyakuliwa na dereva wa timu ya RED BULL MARK WEBBER,nafasi ya nne ikanyakuliwa na JENSON BUTTON.

Lewis Hamilton wa timu ya MACLAREN alishindwa kumaliza mbio hizo kwa mara ya pili mfululuzo baada ya hiyo jana kukwaruzana na WEBBER katika mzunguko wa 36.

Msimamo wa mbio hizo unaonyesha MARK WEBBER anongoza Madera wezake akiwa na Alama 202,huku ALONSO akiwa wa pili na Alama 191,LEWIS HAMILTON yeye NASHIKA nafasi ya tatu akiwa na Alama 182 huku VETTEL akiwa katika nafasi ya nne na Alamaa 177.

Madereva hao watachuana katika mashindano manne yaliyobaki ya GRAND PRIX ili kumpata bingwa WA DUNIA ambayo ni JAPAN,KOREA ya KUSINI,BRAZIL na fainali itakuwa ABU DHABI.

====

No comments:

Post a Comment