Tuesday, September 28, 2010

Miss Tanzania



Miss Tanzania 2010 GENEVIEVA EMMANUEL ameonyesha matumaini kwamba atafanye vema katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia MISS WOLRL ambayo yanatarajiwa kufanyika mjini SANYA nchini china OCTOBA 31 mwaka huu.
GENEVIEVA amesema maadalizi aliyofanya ya kujenga kujiamini,kujieleza na maadalizi ya mwisho mwisho atakayofanya atakapo wasili nchini china yatamsaidia kupata ushindi katika mashindano hayo lakini akakiri kwamba kutakuwa na ushindani mkubwa
Mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania HASHIM LUDENGA amesema Tanzania imefika katika hatua zuri katika jukwaa la urembo kimataifa ingawa wamekuwa hawapati taji la DUNIA kutokana na wasichana wengi kukosa kujiamini.
Miss Tanzania 2010 GENEVIEVA EMMANUEL anaagwa kesho jijini dsm na ataondoka kwenda CHINA keshokutwa siku ya ALHAMIS tayari kwa kinyanganyiro hicho kitakachofanyika CHINA, OCTOBA 31

No comments:

Post a Comment