Tuesday, September 14, 2010

Mafunzo kikapu


Makocha 20 wa mpira wa kikapu wameanza mafunzo kwa vitendo ya mchezo huo yanayotolewa kwa ushirikiano kati ya shirikisho la mpira wa kikapu nchi TBF na shirikisho la mpira wa kikapu la kimataifa FIBA katika viwanja vya DON BOSCO jijini DSM.

Wakizungumza wakati wa mafunzo hayo makamu wa rais wa shirikisho hilo FARESI MAGESA na mkufunzi kutoka FIBA ambaye ni raia wa Kenya SAMWELI WANJOHI wamese mafunzo hayo yatasaidia kupata makocha wengi wa kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wake kocha chipukizi anayehudhuria mafunzo hayo mwanadada CRISTIAN KIMAMLA akizungumza kwa niamba ya wanakozi wazake amesema mafunzo hayo yatasaidia kunua mchezo huo hasa katika shule za msingi na sekondari.

Makocha hao wamejifunza stadi mbalimbali kwa vitendo ambazo ni njisi ya kukaba,kukokota na kutoa pasi na umakini kwa wachezaji wanapokua uwanjani.


No comments:

Post a Comment