Tuesday, September 14, 2010

Makocha wa kikapu mafunzoni


Makocha wa mpira wa mikono wanaohudhuria mafunzo kwa muda wa siku kumi kwenye uwanja wa ndani wa taifa wametakiwa kuyatumia mafunzo hayo kwa ajili ya kuendelea mchezo huo katika mikoa yao.

Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka ubalozi wa Ujerumani PETER HANS amesema Tanzania imechelewa sana kutoa mafunzo kwa makocha wa mpira wa mikono na itachukua kama miaka kumi hivi kufikia mchezo huo kufikia katika kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wao makocha SARA ALLY na JOSON NKONGO wamesema watahakisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi katika shule za msingi na sekondari kwani huko ndio walipo wachezaji.

Makocha ishirini kutoka mikoa ya Kagera,pwani,Dsm,Kilimanjaro,Mtwara,Mbeya,Tabora na Lindi wanahudhuria mafunzo hayo.


No comments:

Post a Comment