Tuesday, September 14, 2010

Makundi ya fainali za Afrika kwa wanawake kupangwa Afrika Kusini wiki ijayo

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake TWIGA STARS CHARLES MKWASA na mwenyekiti wa Chama Soka la wanawake tanzania LINA MHANDO kuhudhuria upangaji wa ratiba ya michuano ya kombe la matifa ya Afrika kwa wanawake jijini JOHNESBURG Afrika Kusini wiki ijayo.
Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF FLORIAN KAIJAGE amesema chama cha soka cha Afrika Kusini SAFA kimeleta barua ya mwaliko kwa wajumbe wa upangaji wa ratiba hiyo na hiyo TFF kuwachangua mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo LINA MHANDO na kocha mkuu wa timu hiyo CHARLES MKWASA kuhudhuria kikao hicho cha CAF cha upangaji wa ratiba.
Kaijage amesema fainali hizo za kombew la matifa ya Afrika kwa wanwake yatashirikisha nchi nane ambazo ni Tanzania,Mali,Ghana,Algeria,Nigeria,Cameroon,Equitoria gene na wenyeji Afrika Kusini na kwamba fainali hizo zitaanza kutimu vumbi kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 14 mwaka huu.
===
Shirikisho la soka nchini TFF limepokea malalamiko kutoka Azam FC juu ya uchezeshaji mbaya wa mchezo kati yao na Simba ulopigwa katika dimba la mkwakwani Mkoani TANGA mwishoni mwa wiki na Azam kulala kwa mabao mawili kwa moja.
Akizungumza na waandishi wa wabari katika Ofisi za shirikisho hilo hii leo, Afisa habari wa TFF, FLORIAN KAIJAGE amesema malalamiko hayo baada ya kupokelewa na sekretarieti ya TFF tayari yamekabidhiwa kwa kamati ya mshindano ya TFF kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi
Ligi kuu ya Tanzania bara inaendelea tena kesho katika viwanja mbalimbali,ambapo mkoani morogoro Yanga watakuwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa sukari wakati mahasimu wao Simba wao wanateremka dimbani dhidi ya JKT RUVU katika dimba la CCM KIRUMBA.

No comments:

Post a Comment