Tuesday, September 21, 2010

BMT wapewa gari


Hatimaye neema katika sekta ya michezo imeenza kujidhihirisha hapa nchini baada ya leo hii shirika la UK SPORT kwa kushirikiana na Tanzania kuzindua kituo cha nne maalumu cha kimataifa cha uongozi wa michezo kwa vijana.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo JOEL BENDERA ambaye ametoa wito wa kutumia furasa hiyo kwa maendeleao ya michezo nchini.

Waweza kuona ni suluhisho la tatizo kubwa la michezo hapa nchini na hii yawezekana endapo tu makusudi na malengo ya kituo hiki yakifanyiwa kazi ipasavyo.

Michezo ni muhimu sana katika maendeleo ya taifa lakini kwa Tanzania hali hiyo bado haijaonekana dhahiri shahir kutokana na kukosa msingi imara wa kukuza wanamichezo chipukizi kwa ajili ya ujenzi wa timu za taifa za michezo mbalimbali za siku za usoni.

Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo, JOEL BENDERA amekiri kufa kwa michezo hapa nchini hasa ngazi za chini vijijini , ilayani hadi mikoani hali inayomfanya sasa avae kibwebwe kwa kuwataka viongozi wa maeneo hayo kuwa watendaji na si wasemaji tu.


Awali NICK DIMKY mwakilisi wa michezo wa shirika la UK SPORT, ameitaka Tanzania kutumia vema fursa hii ili kupata walimu vijana watakaojenga misingi imara ya michezo na hatimaye jina la Tanzania kujulikana katika ulimwengu wa michezo

Hiki ni kituo cha nne kwa Tanzania, miongoni mwa vituo vya Arusha, Songea na Malya na kinasimamiwa na Baraza la Michezo nchini BMT na UK SPORT wametoa msaada wa gari jipya aina ya Toyota kwa ajili ya kurahishisha shughuli za utendaji wake.


No comments:

Post a Comment