Wednesday, September 8, 2010

Michezo ya leo

Katika netiboli timu yetu ya taifa TAIFA QUEENS iliyoko AFRIKA KUSINI kwa mashindano ya mataifa ya AFRIKA, kidogo mambo yamekwenda kombo.

Walianza kwa kuwafunga LESOTHO magoli 50 kwa 25, lakini sasa nao kibao kimewageukia.

Jana imecheza mechi mbili, mechi ya kwanza imechapwa na AFRIKA KUSINI kwa magoli 71 kwa 25.

Kwenye mchezo wa pili TAIFA QUEENS ikachapwa na NAMIBIA kwa magoli 38 kwa 28.

ZIMBABWE wao walishinda mechi yao wakiichakaza LESOTHO kwa magoli 54 kwa 24.

TAIFA QUEENS sasa imebakisha mechi mbili dhidi ya BOTSWANA na ZIMBABWE.

= = =

Katika kandanda,Timu ya taifa ya ARGERTINA imeibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-1 dhidi ya mabingwa wa dunia HISPANIA katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa jana kwenye dimba la Monumental.

MAGOLI ya ARGENTINA yalipachikwa wavuni na Carlos Teveza aliyefunga mabao mawili huku bao la tatu na la nne ya Argertina yakiwa yamefungwa na Gonzalo Higuain na Serio Aguero,Hispania ikajipatia goli la kufutia majozi kupitia kwa Fernando Llorente dakika sita kabla ya mpira kumalizika.

Kocha wa HISPANI Vicente del Bosque amekisifu kikosi cha Argertina kwamba kilicheza vyema kuliko walivyocheza kwenye fainali za konbe la dunia zilizomalizika nchini Afrika kusini JULY huku HISPANIA wakitawazwa mabingwa wapya wa kombe la dunia 2010

==

Kocha ENGLAND, FABIO CAPELO amesema amepata faraja kubwa kwa timu yake kufanya vyema kwa mchezo wa pili dhidi ya USWIS na sasa anaiona njia nyeupe ya kushiriki fainali za kombe la mataifa Ulaya 2012.

Katika mchezo wa jana ENGLAND iliichapa USWIS mabao 3-1,magoli ya England yakikwamishwa wavuni na WAYNE ROONEY, ADAM JOHNSON na DAREN BENT huku bao la kufutia machozi kwa USWIS likifungwa na HERDAN SHAQIR.

Katika michezo mingine URENO ikalala kwa bao moja kwa bila dhidi ya NORWAY, UHOLANZI ikaichapa FINLAND kwa magoli MAWILI kwa MOJA.UFARANSA wakaichapa BOSNIA HERZEGOVINA kwa magoli MAWILI kwa BILA.

UJERUMANI ikaikandamiza AZERBAIJAN kwa magoli 6-1 huku ITALY ikiichapa VISIWA vya FAROE kwa magoli MATANO kwa BILA, CROTIA na UGIRIKI nao wametoshana nguvu bila ya kufungana.

===

katika machiuno ya wazi ya Marekani maarufu kama US OPEN VENUS WILLIAMS ameibuka kidedea baada ya kumfunga FRANCESCA SCHIAVONE,kwa seti mbili kwa bila ya 7-6, 6-4.

KIM Clijsters ameshinda kwa seti 2-1 ya 6-4 5-7 6-3 dhidi ya SAM STOSUR na sasa KIM Clijsters atakutana na VENUS WILLIAMS katika nusu fainali ya michuano hiyo.

Kwa upande wa wanaume STANISLAS Wawrinka amemfunga Sam Querrey kwa ushindi wa 7-6, 6-7, 7-5 na sasa atachuana katika robo fainali na Mikhail Youzhny wa Urusi ambaye alimchapa Tommy Robredo wa Hispani kwa seti 2-1 ya 7-5, 6-2 na 4-6.

Mchezo mwingine ulishuhudia Fernando Verdasco akimchapa David Ferrer kwa ushindi wa 5-7, 6-7na 7-6 na sasa atakutana na Rafael Nadal katika robo fainali.

NADAL ametinga hatua hiyo baada ya kumchapa Feliciano Lopez kwa ushindi wa seti 3-0 ya 6-3 6-4 6-4.

===

Michuano ya kombe la dunia ya mpira wa kikapu bado inaendelea ISTANBULL huko UTURUKI.

Argetina imeichapa Brazil kwa pointi 93 kwa 89 na kutinga katika hatua ya Robo fainali.

Katika mchezo mwingine LITHUANIA ikaichapa CHINA kwa pointi 78 kwa 67

Kwa matokeo haya LITHUANIA watacheza na ARGENTINA kwenye mechi ya robo fainali ya kwanza, huku MAREKANI wakicheza na URUSI,UTURUKI wakicheza na SLOVENIA na mabingwa wa ULAYA HISPANIA wakicheza na SERBIA.

Mwisho wa habari za michezo na burudani kwa mchana wa leo, kwa habari nyingine kemkem za michezo usikose kujiunga nasi saa 1;30 jioni hapa TBC TAIFA.

= =

No comments:

Post a Comment