
washiriki wa big brother all stars wakipeyana moyo
Timu ya soka ya Filbert Bayi leo inateremka dimbani kuchuana na mabingwa watetezi ST.MERYS KITENDE ya Uganda katika nusu fainali ya kwanza mchezo utakaochezwa mjini Nakuru nchini Kenya.
Nusu fainali ya pili katika soka inazikutanisha timu za soka za ST.MARKS ya Kenya itakayoshuka dimbani kumenyana na PS BABTIST ya Rwanda.
Katika netiboli timu ya Filbert Bayi inashuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya shule ya sekondari BLESSED SACRAMENT KIMAYA YA UGANDA huku nusu fainali ya pili ikizikutanisha ST.MERYS KITENDE ya Unganda dhidi ya SHIMBA HILL YA KENYA.
Timu za Tanzania katika michezo ya mpira wa kikapu,mikono na Voliboli zote zimeshindwa kutamba na kuitinga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
===
Timu za kriketi za klabu ya Gymkhana ya Tanzania na ile ya jeshi la wanamaji la India zimechuana katika mchezo maalumu wa kuendeleza uhusiano wa kimichezo kati ya Tanzania na India,mechi hiyo imechezwa hii leo katika viwanja vya Gymkhana jijini DSM
mwenyekiti wa kriketi wa klabu ya Gymkhana KULBIR CUPTA na Nahodha wa timu ya wanamaji India DINESH TRIPATHI wamesema michezo hujenga urafiki na uhusiano mwema kwa wachezaji na nchi kwa ujumla
Meli ya kivita ya wanamaji wa jeshi la india imewasili Dar es Salaam hiyo jana ikiwa na lengo la kulinda amani katika bahari ya hindi.
===
Wachezaji kutoka katika vilabu sita vya gofu wamechuana hii leo kwa lengo la kuchangua wachezaji wa akiba wa timu ya taifa ya GOFU ya Tanzania.
Afisa tawala wa Chama cha gofu Tanzania TGU, SOPHIE NYANJERA, amesema wameamua kuwashindanisha wachezaji wa timu ya taifa ya Gofu na wale ambao hawapo katika timu hiyo kwa madhumuni ya kupima viwango vyao
Kwa upande wake kocha wa timu ya taifa ya GOFU FARAYI CHITENGWA amesema amefurahishwa na kiwango cha uchezaji kilicho onyeshwa na wachezaji walio nje ya timu ya taifa na ni hazina kwa timu ya taifa
Wachezaji kutoka klabu za Gymkhana DSM, ARUSHA, MFINDI na Morogoro,TPC na LUGALO wamechuana katika mashindano hayo.
===
Katika klabu bingwa Afrika timu ya Heartland ya Nigeria imenashuka dimbani kuchuana na Ismaili ya Misri mchezo utakaopingwa kwenye uwanja wa Dan Anyiam wakati katika mchezo mwingine wa kundi B Al Ahly ya MISRI itaonyeshana kazi na JS Kabylie
Msimamo kabla ya mchezo wa leo JS Kabylie inaongoza ikiwa na pointi 9 kibindoni ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi 4, Ismaili inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 3 wakati Heartland inaburuza mkia ikiwa na pointi 1
Katika kundi A Entente Setif imeinyuka Dynamos ya Zimbabwe kwa mabao matutu kwa bila huku mabingwa watetezi TP Mazembe wanateremka dimbani kumenyana na Esperance
Msimamo katika kundi A mabingwa watetezi TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa imejikusanyia pointi 7 wakati Esperance inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, E. Setif inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4 wakati Dynamos inaburura mkia ikiwa na pointi zake 3.
====
Ligi kuu ya ENGLAND imeendelea hii leo kwa michezo minne kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali,Aston Villa wamewakaribisha Everton katika uwanja wao wa nyumbani wa Villa Park huku Bolton wakimenya na Birmingham katika dimba la Reebok.
Michezo mingine majogoo wa jiji Liverpool wameshuka dimbani dhidi ya West Brom katika uwanja wake wa nyumbani wa AN FIELD huku Sunderland wakiwakaribisha Man City.
Katika michezo iliyochezwa jana ARSENAL ilichapa Black BURN kwa mabao 2-1huku mashetani wekundu MANCHESTER UNITED wakatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa OLD TRAFORD na kuichapa WEST HAM UNITED kwa mabao matatu kwa bila.
Michezo mingine iliyochezwa jana mabingwa watetezi CHESLEA walitoka kifua mbele baada ya kuinyuka STOKE CITY kwa mabao MAWILI kwa sifuri huku BLACK POOL ikitoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na FULHAM wakati WOLVESHAMPTON ikakabana koo na NEWCASTLE na kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.
===
STARS yaanza mazoezi kuivaa Algeria.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars kilichotangaza na kocha wake mkuu JAN POULSEN jijini Arusha hiyo jana kinaanza mozezi hii leo katika uwanja wa karume tayari kuikabili Algeria ungenini Septemba 4.
Katika kikosi kilichotangazwa jana hakina mabadiliko licha ya kocha huyo kushuhudia michezo miwili mikubwa,mchezo kati ya watani wa jadi Simba na Yanga uliopingwa siku ya jumatano kwania Ngao ya Hisani uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini DSM na ule wa uliopingwa katika uwanja wa Shekh Amr Abeid kati ya AFC na Azam FC.
POULSEN amerudisha kikosi kilekile kilichocheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars mchezo ulipingwa AUGOSTI 11 katika uwanja wa Taifa jijini DSM na timu hizo kufungana bao moja kwa moja ikiswa ni pamoja na mlinda mlango majeruhi JUMA KASEJA na kumuacha kiungo wa pembeni KIGI MAKASI.
Pia POULSEN amewateua katika timu yake wachezaji wanosukuma soka ya kulipwa Nizar Khalifan anayekipinga katika timu ya Vancouver White Caps ya Canada,Henry Josoph anayecheza Sweden, Danny Mrwanda anayecheza Veitnam na Idrisa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya.
Star itashuka dimbani kuikabili Algeria ugenini Septemba 4 kabla ya kuikabili MORROCCO Octoba 9 jijini DSM.
Stars imepangwa kundi moja na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Morocco na Algeria.
==
Ligi kuu ya Tanzania bara yasimama kuipisha Stars.
Ligi kuu Tanzania bara iliyoanza kutimua vumbi katika viwanja sita siku ya jumamosi imesimama hadi septemba 11 kuipisha Taifa Stars inayojianda kuteremka dimbani dhidi ya Algeria ugenini Septemba 3.
Katika michezo iliyochezwa juzi,Katika dimba la Uhuru mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Simba ukipenda waiti wekundu wa masimbazi wao waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya African Lyon.
Kwingineko mabingwa wa Ngao ya Hisani Yanga ilibuka kidedea baada ya kuichapa Polisi Tanzania kwa bao moja kwa bila.
Katika uwanja wa Shekh Amri Abeid jijini Arusha wanalambalamba AZAM FC iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya AFC.
Huko Mwanza wana kishamapanda Toto Africans ya Mwanza wakatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba na kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi timu iliyopanda daraja ya Ruvu Shooting.
Huko Kagera Ruvu JKT waliwachapa wenyeji wao KAGERA SUGAR bao moja kwa bila wakati Mtibwa Sugar waliifunga Majimaji ya Songea bao moja kwa bila,
== =
Mashindano ya ngumi ya Afrika ya Mashariki kuanza kesho
Mashindano ya ngumi za riadhaa ya Afrika ya Mashariki maarufu kama mabingwa wa mabingwa yanaanza kutimua vumbi hapo kesho jijini DSM huku mabondia wa Tanzania wakitamba kufanya vyema katika mashindano hayo.
Akizungumza na TBC kwa njia ya simu katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT) MAKORE MASHANGA amesema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika huku nchi zitakazo shiriki zikitazamiwa kuwasili jioni ya leo
Mashindano hayo yanashirikisha mabondia kutoka katika nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi ,Botwana na Morius na wenyeji Tanzania.
===
Mashindano ya UMISETA kwa timu za Afrika ya Mashariki yaanza nchini Kenya
Mashindano ya UMISETA kwa timu za Afrika Mashariki yameanza nchini Kenya huku timu za Tanzania zikianza kutupa karata zao za kwanza asubuhi ya leo.
Akiongea na TBC kwa njia ya simu mratibu wa UMISETA kwa timu za Tanzania SALUM SALUM amesema timu ya soka ya wasichana wa Tanzania imeteremka dimbani kuchuana na RWANDA.
SALUM amezitaja timu nyingine za Tanzania zitakazoshuka dimbani kuwa ni timu ya mpira wa kikapu itakayomenyana na Uganda, timu ya mpira wa wavu ya wasichana inaikabili timu ya SUDAN na timu ya mwisho kucheza itakuwa ni ya soka ya wanaume ya Tanzania itakayocheza na Kenya.
Mashindano hayo ya UMISETA ya Afrika Mashariki yanashirikisha timu kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda, Burundi na wenyeji Kenya,.
====
Liverpool uso kwa uso na Manchester city
Lgi kuu ya Uingereza itaendelea usiku wa leo kwa matajiri wapya wa ligi hiyo MANCHESTER CITY itakapowakatibisha majogoo wa jiji LIVERPOOL katika uwanja wa CITY OF MANCHESTER.
Kocha wa Liverpol ROY HOGSON anaamini vijana wake watacheza vizuri ugenini na kuibuka na ushndi katika mchezo huo huku kocha wa Man City ROBERTO MANSHINI akijigamba kuibuka kidedea katika uwanja wake wa nyumbani kwa usajili wa nguvu alioufanya msimu huu.
Katika michezo iliyochezwa jana Mashetani wekundu Manchester United walijikuta wakilazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya wenyehi wao FULHAM waliokua chini ya kocha wao mpya MARK HUGHES.
MANCHESTER ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lilofungwa na mgongwe PAUL SKOZI katika dakika ya 12 ya mchezo.
FULHAM wakaja juu katika kipindi cha pili na kusawazisha bao hilo kupita kwa DAVIS lakini MAN UNITED wakajipatia bao la pili baada ya beki wa FULHAM BREDE HANGALEND kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona
LUIS NANI akaikosesha MAN UNITED bao la tatu na pengine lingekua la ushindi lakini penati yake aliyopinga zikiwa zimesalia dakika sita mpira kumalizika ikaenda mikononi mwa kipa wa FULHAM, DAVID STOCKDALE.
Fulham wakafanya shambulizi la mwisho na kupata kona ambayo ilizaa bao lilofungwa na beki wake BREDE HANGALEND.
Katika mchezo mwingine ulichezwa jana ASTON VILLA ilipata kichapo cha mabao sita kwa bila kutoka kwa timu ya NEW CASTLE UNITED
== =
Federer Bibgwa wa Western and Southern Masters
ROGER FEDERER ameshinda taji lake kubwa la 17 la tenisi baada ya kumchapa Mmarekani MARDY FISH kwa ushindi wa seti 2-1 ya 6-7,7-6 na 6-4 katika mchezo wa fainali iliyokua ya kusisimua ya WESTERN AND SOUTHERN FINANCIL GROUP MASTERS iliyofanyika jana nchini MAREKANI.
FEDERER mchezaji nambari mbili kwa ubora wa tenisi duniani ilibidi afanye kazi ya ziada kumdhiibiti mpinzani wake FISH baada ya kufungwa katika seti ya kwanza kwa 7-6.
FEDERER alikuja juu na kucheza kwa ustadi mkubwa na kushinda katika seti ya pili na ya tatu baada ya kupata shindi kwa seti 7-6 na 6-4.
Hili ni taji la NNE la WESTERN AND SOUTHERN FINANCIL GROUP MASTERS kwa FEDERER na likiwa ni taji lake la 17 la mashindano makubwa akiwa nyuma ya Mmarekani ENDRE AGASS mwenye mataji 18.
===
Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Meryl
STARS ya kuivaa Al-geria yatangazwa
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars JAN POULSEN anatangaza kikosi cha timu hiyo jijini Arusha hii leo kitakacho ivaa Algeria ugenini Septemba 4.
Kikosi hicho kitaingia kambini jijini DSM kesho tayari kwa mazoezi ya kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.
Katika kikosi kitakacho tangazwa leo haitarajiwi kama kocha huyo atafanya mabadiliko makubwa licha ya kushuhudia michezo miwili,mchezo kati ya watani wa jadi Simba na Yanga uliopingwa siku ya jumatano kwania Ngao ya Hisani uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini DSM na ule wa jana uliopingwa katika uwanja wa Shekhe Amur Abed kati ya AFC na Azam FC.
Wachambuzi wa mambo ya michezo wanasema kocha atarudisha wachezaji wale wale aliowaita kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars mchezo ulipingwa AUGOSTI 11 katika uwanja wa Taifa jijini DSM na timu hizo kufungana bao moja kwa moja.
Pia POULSEN anatarajiwa kuwateua katika timu yake wachezaji wanosukuama soka ya kulipwa ambao ni Nizar Khalifan anayekipinga katika timu ya Vacouvor White Camps ya Canada,Henry Josophy anayecheza Sweeden na mshambuliaji wa timu hiyo Danny Mrwanda anayecheza Veitnam na Idrisa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya.
Star ikishashuka dimbani dhidi ya Algeria ugenini Septemba 4 itakabiliwa na mtihani mwingine mgumu nyumbani dhidi ya timu ngumu ya MORROCCO Octoba 9.
Timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars imepangwa katika kundi lenye timu za Jamhuri ya Afrika ya Kati,Morocco na Algeria.