Wednesday, August 11, 2010

STARS yashindwa kutamba nyumbani

Timu ya taifa ya Tanzania-TAIFA STARS imelazimisha sare ya goli MOJA kwa MOJA dhidi ya timu ya taifa ya KENYA-HARAMBEE STARS katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa UHURU jijini DSM.
Katika mchezo huo wa kwanza kwa kocha mpya wa STARS- JAN PAULSEN ,HARAMBEE STARS ndio waliokuwa wa kwanza kupachika bao kupitia kwa kiungo wao anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya INTER MILAN nchini ITALIA-MCDONALD MARIGO katika dakika ya 13 huku STARS wakibanwa kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili STARS walibadilika na kucheza soka la malengo zaidi hasa baada ya kocha PAULSEN kufanya mabadiliko hususani kwenye safu ya kiungo ambapo dakika ya 57 kiungo mshambuliaji MRISHO KHALFAN NGASSA aliisawazishia STARS bao hilo na kufanya matokeo kuwa sare ya goli MOJA kwa MOJA hadi mwisho wa mchezo.
Mara baada ya mchezo huo kiungo wa HARAMBEE STARS-MCDONALD MARIGA na kiungo wa TAIFA STARS ATHUMANI IDD CHUJI walizungumza na mwandishi wa TBC kuhusu mchezo huo
Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa leo ambapo ni kwa mujibu wa kalenda ya shirikisho la soka duniani -FIFA ,timu ya taifa ya BRAZIL imeilaza MAREKANI magoli MAWILI kwa BILA yakifungwa na NEYMAR pamoja na ALEXANDER PATO,huku NIGERIA ikinyukwa magoli MAWILI kwa MOJA na JAMHURI YA KOREA.
Mechi nyingine zinazochezwa usiku huu ni kati ya AFRIKA KUSINI na GHANA,ANGOLA dhidi ya URUGUAY,ENGLAND na HUNGARY,NORWAY wakiumana na UFARANSA ,DENMARK wao wakichuana na UJERUMANI huku bingwa wa dunia HISPANIA wakikwaruzana na MEXICO.

No comments:

Post a Comment