Tuesday, August 24, 2010

Bondi ya Utalii Tanzania TTB imepanga kutumia shilingi milioni mia nane kutanganza vivutio vya utalii katika ligi kuu ya soka ya Uingereza.
Mkurungezi wa mtendaji wa TTB, ALOYCE NZUKI amesema bodi ya Utalii Tanzania katika harakati zake za kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kimataifa imenunua nafasi ya kutangaza kwenye viwanja vya nyumbani vya timu sita zilizopo kwenye ligi kuu ya UINGEREZA kwa michezo 114 kuanzia AUGOSTI 14 hadi MAY 22 mwakani (PAUSE)

NZUKI alivitaja viwanja na timu hizo sita kuwa ni BLACKBURN ROVERS inayaotumia uwanja wa EWOOD PARK,NEWCASTLE UNITED inayotumia uwanja wa ST.JAMES PARK,STOKE CITY inayotumia dimba la BRITANIA,SUNDERLAND inayotumia uwanja wa LIGHT,WEST BROMWICH ALBION inayotumia uwanja wa THE HAWTHORNS na WOLVERTHAMTON inayotumia dimba la MALINEUX.

NZUKI mesema vivutio vya utalii vinavotangazwa katika viwanja hivyo ni Mlima KILIMANJARO, ZANZIBAR na SERENGETI na tayari matangazo hayo yameonekana katika mchezo kati ya BLACKBURN ROVERS dhidi ya EVERTON uliochezwa kwenye dimba la EWOOD PARK AUGOSTI 14.

==

Watani wa jadi,klabu za Simba na Yanga zimegomea mgao wa shilingi milioni THELATHINI NA MBILI kwa kila timu uliotokana na mechi ya Ngao ya Hisani na kudai hauendani na gharama za maandalizi ya mchezo huo.

Afisa Habari wa Simba CLIFORD NDIMBO na yule wa Yanga LUIS SENDEU wamesema timu zao haziko tayari kuchukua mgawanyo huo na endapo TFF haitachukua uamuzi wa kuuboresha uendane na kusudiao lao kuna uwezekano mkubwa wa timu hizo kugoma kuendelea kushiriki ligi kuu Tanzania Bara.
Klabu hizo zimedai kutokuwa na imani na shirikisho la soka nchini TFF, kufuatia kuendelea kutotendewa haki katika mapato hasa michezo inayozikutanisha timu hizo mbili ambayo huingiza mapato mengi kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wa soka wanaojitokeza uwanjani kushuhudia mpambano kila timu hizo zinapoteremka dimbani kuchuana.
katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliopigwa Jumatano iliyopita katika uwanja wa taifa jijini DSM jumla ya shilingi milioni MIA MBILI NA ISHIRINI NA MBILI zilipatikana lakini klabu hizo zimeambulia mgao wa shilingi milioni 32 kila moja.

====
Aliyekuwa Kanali wa jeshi la kujenga taifa kikosi cha TAU MGULANI na mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa mikono AFRIKA MASHARIKI NA KATI CECILIUS FUSI ambaye amefariki dunia jumapili iliyopita mwili wake unatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya kinondoni Jijini DSM.

Wakizungumza katika msiba huo baba wa marehemu EDWARD FUSI na MARIETA FUSI wamesema msiba huo ni pigo kwa familia pamoja na watu wa करिबू
Baba wa marehemu FUSI amesema wanatarajia kuzika mwili wa marehemu CECILIUS FUSI kesho baada ya watoto wa marehemu ambao wanaishi nje ya nchi kuwasili nchini hii leo lakini iwapo hawatowasili mazishi yatafanyika na baadaye msiba utahamishiwa mjini Songea kwa wazazi wa marehemu.
Marehemu atakumbukwa kwa kuhimiza michezo ambapo kabla ya kifo chake alikuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika Mashariki na Kati.
Marehemu amecha mke DORIS FUSI pamoja na watoto tisa.

=====

MASHINDANO ya kimataifa ngumi za ridha maarufu kama mabingwa wa mabingwa yanaanza mchana huu katika ukumbi wa DDC MLIMANI CITY jijini DSM huku mashindano hayo yakiwa yanakabiliwa na ukata mkubwa ngumi kifedha.
Mashindano hayo yanashirikisha nchi SITA, zikiwemo, KENYA, UGANDA, RWANDA, BOTSWANA, MAURITIUS na wenyeji TANZANIA.
Ukata wa fedha unatokana na mabondia kutoka nchini KENYA na UGANDA kutolewa katika Hotel waliokuwa wamefikia na kuhamishiwa Hotel ya bei rahisi.
==
BINGWA wa mchezo wa Golf duniani TIGER WOODS ametalikiana na mkewe ELIN NORDEGREN.
Hayo yamefahamika katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa mchezaji golf huyo namba moja duniani.
Kila mmoja alibainisha kwa kudai kuwa wanasikitika kuwa ndoa yao imefikia tamati na kutakiana kila la heri .
Hata hivyo wanasema watasaidiana majukumu ya kulea watoto wao wawili.
Suala la kugawana fedha bado halijawekwa wazi lakini taarifa katika vyombo vya habari nchini MAREKANI zinasema NORDEGREN huenda akaondoka na dola za kimarekani MILIONI 100.
WOODS amekuwa na matatizo kwenye ndoa yake baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.
==

NAIBU waziri mkuu wa ENGLAND, NICK CLEGG amewaambia wakaguzi wa viwanja wa FIFA kuwa ENGLAND ni zaidi ya nchi nyingine zilizoomba kuandaa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018.
CLEGG, ameaysema hayo wakati maofisa hao wa FIFA wakiwa nchini humo kwa siku NNE kukagua baadhi ya viwanja na baadae kutoa ripoti kama ENGLAND wataweza kuandaa au la.
DESEMBA 2 mwaka huu waandaaji wa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 na 2022 watatajwa ambapo kwa mwaka 2014 nchi ya BRAZIL ndiyo itakayoandaa mashindano hayo baada ya mwaka huu kufanyika nchini AFRIKA KUSINI kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika.
Katika kupambana na uandaaji wa mashindano hayo inaonekana ENGLAND imekuwa ikipata upinzani mkubwa kutoka kwa nchi ya URUSSI.
Ujumbe wa watu SITA ukiongozwa na rais wa chama chya soka nchini CHILE, HAROLD MAYNE-NICHOLLS ulipata fursa ya kutembea kutoka eneo la DOWNING STREET hadi uwanja wa WEMBLEY ambapo walikutana na kocha wa timu ya taifa ya ENGLAND, FABIO CAPELLO.
Viwanja ambavyo vinaangaliwa na wakaguzi hao ni pamoja na kile cha OLYMPIK, uwanja wa ARSENAL wa EMIRATES, WHITE HART LANE, MK, NOTTINGHAM FOREST.
==

MCHEZAJI wa TENNIS wa DENMARK, CAROLINE WOZNIACKI amefanikiwa kuibuka na ushindi katika mashindano ya kombe la ROGERS kwa kumshinda VERA ZVONAREVA kwa seti 6-3 6-2.
Kila upande uliweza kuanza vizuri kwa kushambuliana kabla ya WOZNIACKI kubadili mchezo na kuanza kupata pointi za mfululizo.
Kabla ya mchezo huo WOZNIACKI alifanikiwa kumfunga SVETLANA KUZNETSOVA katika mchezo uliocheleweshwa kutokana na mvua.
WOZNIACKI kwa sasa anashikilia namba MBILI kwa ubora wa kiwango cha TENNIS.
==

No comments:

Post a Comment