.jpg)
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kikosi cha wachezaji 25 wa timu hiyo wanaoanza kambi kesho, Kocha mkuu wa TWIGA STARS, CHARLESE MKWASA, amesema wameamua kuanza kambi mapema igawa hawajui tarehe ya kuanza kwa mashindano hayo ya Afrika kwa wanawake.
Mkwasa amesema TWIGA STARS,itacheza na Banyana Banyana septemba 29 na Oktoba 2 na pia itacheza dhidi ya ZIMBABWE Octoba 6 na 10 kwa lego la kuiweka sawa timu hiyo kabla ya mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa wanawake na kwamba michezo hiyo itachezwa jijini DSM.Fainali za soka kwa mataifa ya Afrika kwa wanawake yatazishirikisha timu za taifa za Algeria,Ghana,Tunisia,Equitoria Gine,Tanzania,Cameroon na wenyeji Afrika ya Kusini na yanatarajiwa kutimua vumbi mwezi Okatoba
No comments:
Post a Comment