Wednesday, August 25, 2010



MABARAZA ya michezo ya BMT na BMZ yametakiwa kufanya jitihada za kusuluhisha mgogoro wa vyama vya mchezo wa NETIBOLI visiwani ZANZIBAR na ule wa TANZANIA BARA.

Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, SETH KAMUHANDA ametaka mgogoro huo umalizwe kwa faida ya mchezo huo

Katika kambi ya mazoezi inayojiandaa na mashindano ya kimataifa nchini AFRIKA KUSINI mwezi ujao , ni wachezaji wa TANZANIA BARA pekee ambao wapo katika kambi hiyo huku wachezaji kutoka ZANZIBAR wakiwa hawajaripoti katika kambi hiyo kutokana na madai yaliyochangiwa na mgogoro wa viongozi wa CHANEZA na CHANETA.

Katika hatua nyingine, katibu KAMUHANDA ametolea ufafanuzi kuwa timu ya soka ya wanawake ya TWIGA STARS wanaidai shirikisho la soka nchini TFF malimbikizo yao ya fedha ya nyuma na hayahusiani na msaada uliotolewa na rais JAKAYA KIKWETE kwa timu hiyo.

Fedha ambazo rais KIKWETE ametoa kama msaada kwa timu hiyo ni MILIONI HAMSINI fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kambi ya matayarisho ya timu hiyo inayojiandaa na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini AFRIKA KUSINI mwezi OKTOBA mwaka huu.

No comments:

Post a Comment