Tuesday, August 31, 2010

Kocha wa netball kuwasili kesho


Kocha wa timu ya taifa ya netiboli SIMONE MACKIMIS kutoka Australia anawasili nchini kesho tayari kwa kuinoa timu hiyo inayojiandaa kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika ya Kusini mwezi ujao.
Kaimu Katibu mkuu wa CHANETA, ROSE MKISI, amesema kocha SIMONE MACKIMIS atakapo wasili atajiunga moja kwa moja na kambi ya timu hiyo ambayo ipo katika shule ya sekondari ya FILBERT BAYI KIBAHA, tayari kwa kuinoa kablya kuondoka kwenda Afrika ya Kusini.
MKISI amesema igawa kocha MACKIMIS atakua na muda mfupi wa kuinoa timu hiyo lakini wanamatumaini kwamba mafunzo atakayotoa yatasaidia timu hiyo kufanya vyema katika mashindano hayo ya Afrika.
Hii itakuwa nia mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya netiboli kunolewa na kocha wa kingeni na kwamba kama walivyo makocha wa soka,ngumi na riadha kocha MACKIMIS pia atalipwa mshahara na serikali.


No comments:

Post a Comment