Wednesday, August 25, 2010


SHIRIKISHO la Kimataifa linalojihusisha na mazoezi ya mwili, viungo na utoaji wa elimu ya michezo la TAFISA linakusudia kutekeleza miradi ya ushirikiano na TANZANIA kupitia chuo cha Maendeleo ya michezo cha MALYA kilichopo mkoani MWANZA.

Katibu mkuu wa shirikisho la michezo kwa wote duniani, WOLFGANG BAUMANN ambaye alitembelea chuo hicho wakati wa ziara yake nchini, ambapo pia kikao cha bodi ya shirikisho hilo kilifanyika jijini DSM.

Aidha , BAUMANN amesema ndani ya chuo hicho cha MALYA kutakuwa na taasisi maalum ya utoaji wa mafunzo kwa vijana, mpango ambao utaanza mwanzoni mwa mwaka ujao na utakuwa na faida kwa nchi zilizopo katika ukanda wa nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla.
==

No comments:

Post a Comment