Sunday, August 29, 2010




Timu ya soka ya Filbert Bayi leo inateremka dimbani kuchuana na mabingwa watetezi ST.MERYS KITENDE ya Uganda katika nusu fainali ya kwanza mchezo utakaochezwa mjini Nakuru nchini Kenya.

Nusu fainali ya pili katika soka inazikutanisha timu za soka za ST.MARKS ya Kenya itakayoshuka dimbani kumenyana na PS BABTIST ya Rwanda.

Katika netiboli timu ya Filbert Bayi inashuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya shule ya sekondari BLESSED SACRAMENT KIMAYA YA UGANDA huku nusu fainali ya pili ikizikutanisha ST.MERYS KITENDE ya Unganda dhidi ya SHIMBA HILL YA KENYA.

Timu za Tanzania katika michezo ya mpira wa kikapu,mikono na Voliboli zote zimeshindwa kutamba na kuitinga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

===


Timu za kriketi za klabu ya Gymkhana ya Tanzania na ile ya jeshi la wanamaji la India zimechuana katika mchezo maalumu wa kuendeleza uhusiano wa kimichezo kati ya Tanzania na India,mechi hiyo imechezwa hii leo katika viwanja vya Gymkhana jijini DSM

mwenyekiti wa kriketi wa klabu ya Gymkhana KULBIR CUPTA na Nahodha wa timu ya wanamaji India DINESH TRIPATHI wamesema michezo hujenga urafiki na uhusiano mwema kwa wachezaji na nchi kwa ujumla

Meli ya kivita ya wanamaji wa jeshi la india imewasili Dar es Salaam hiyo jana ikiwa na lengo la kulinda amani katika bahari ya hindi.

===

Wachezaji kutoka katika vilabu sita vya gofu wamechuana hii leo kwa lengo la kuchangua wachezaji wa akiba wa timu ya taifa ya GOFU ya Tanzania.

Afisa tawala wa Chama cha gofu Tanzania TGU, SOPHIE NYANJERA, amesema wameamua kuwashindanisha wachezaji wa timu ya taifa ya Gofu na wale ambao hawapo katika timu hiyo kwa madhumuni ya kupima viwango vyao

Kwa upande wake kocha wa timu ya taifa ya GOFU FARAYI CHITENGWA amesema amefurahishwa na kiwango cha uchezaji kilicho onyeshwa na wachezaji walio nje ya timu ya taifa na ni hazina kwa timu ya taifa

Wachezaji kutoka klabu za Gymkhana DSM, ARUSHA, MFINDI na Morogoro,TPC na LUGALO wamechuana katika mashindano hayo.

===

Katika klabu bingwa Afrika timu ya Heartland ya Nigeria imenashuka dimbani kuchuana na Ismaili ya Misri mchezo utakaopingwa kwenye uwanja wa Dan Anyiam wakati katika mchezo mwingine wa kundi B Al Ahly ya MISRI itaonyeshana kazi na JS Kabylie

Msimamo kabla ya mchezo wa leo JS Kabylie inaongoza ikiwa na pointi 9 kibindoni ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi 4, Ismaili inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 3 wakati Heartland inaburuza mkia ikiwa na pointi 1

Katika kundi A Entente Setif imeinyuka Dynamos ya Zimbabwe kwa mabao matutu kwa bila huku mabingwa watetezi TP Mazembe wanateremka dimbani kumenyana na Esperance

Msimamo katika kundi A mabingwa watetezi TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa imejikusanyia pointi 7 wakati Esperance inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, E. Setif inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4 wakati Dynamos inaburura mkia ikiwa na pointi zake 3.

====

Ligi kuu ya ENGLAND imeendelea hii leo kwa michezo minne kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali,Aston Villa wamewakaribisha Everton katika uwanja wao wa nyumbani wa Villa Park huku Bolton wakimenya na Birmingham katika dimba la Reebok.

Michezo mingine majogoo wa jiji Liverpool wameshuka dimbani dhidi ya West Brom katika uwanja wake wa nyumbani wa AN FIELD huku Sunderland wakiwakaribisha Man City.

Katika michezo iliyochezwa jana ARSENAL ilichapa Black BURN kwa mabao 2-1huku mashetani wekundu MANCHESTER UNITED wakatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa OLD TRAFORD na kuichapa WEST HAM UNITED kwa mabao matatu kwa bila.

Michezo mingine iliyochezwa jana mabingwa watetezi CHESLEA walitoka kifua mbele baada ya kuinyuka STOKE CITY kwa mabao MAWILI kwa sifuri huku BLACK POOL ikitoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na FULHAM wakati WOLVESHAMPTON ikakabana koo na NEWCASTLE na kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

===


No comments:

Post a Comment