Sunday, August 22, 2010

Simba na Yanga zaanza ligi kuu kwa kishindo

Ligi kuu Tanzania bara imeanza kutimua vumbi katika viwanja sita tofauti kwa timu zote kumi na mbili kushuka viwanjani kuwania pointi mbili muhimu na kujikita kileleni katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu ikiwa ni sihara ya kutaka kutwaa ubingwa wa lkigi hiyo.

Katika uwanja wa Uhuru mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Simba ukipenda waeti wekundu wa masimbazi wao waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya African Lyon mchezo uliokuwa mkali na wakusisimua uliopingwa katika dimba la Uhuru jijini DSM hiyo jana.

Magoli ya Simba hiyo jana yalikwamishwa wavuni na beki wa kushoto wa timu hiyo ambaye amehamia kutoka mahasimu wao Yanga,bao la kwanza akifunga katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza baada ya kuunganisha mpira wa kona ulochongwa na Abdulhalim Umur akicheza mchezo wake wa kwanza tangu ahamie Simba akitokea vijana wa Manungu maarufu kama wakata miwa Mtibwa Sugar.

Mafutah alifunga bao la pili kwa mkwaji wa penati baada ya kiungo mshambuliaji na nahodha wa Simba Nico Nyagawa kuangushwa na mlinda mlango wa African Lyon IVO MAPUNDA na bila ajizi Mafutaha alipinga penati kwa ustadi mkubwa na mkwaju wake kwenda moja kwa moja wavuni katika dakika ya 62 ya mchezo.

Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phir amesema yeye amevutiwa na kiwango cha wachezaji wake walichoonyesha hasa baada ya siku ya jumatano kupoteza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya mahasimu wao Yanga, mchezo uliochezwa kwenye dimba la Taifa jijini DSM ambapo Yanga walishinda mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-1.

Kwa upande wake kocha wa timu ya African Lyon inayomilikiwa na mwanamama RAHAM Al-Harusi Jumanne Chale amesema vijana wake walijitahidi kucheza vyema lakini bahati haikua yao ila akasema atahahakikisha atarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ili kufanya vyema katika michezo ijayo.

Kwingineko mabingwa wa Ngao ya Hisani Yanga imeibuka kidedea baada ya kuichapa Polisi Tanzania kwa bao moja kwa bila bao pekee la Yanga likifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo na Taifa Stars, Jerry Tegete wakati katika uwanja wa Shekhe Amur Abed jijini Arusha matajiri wa jiji la DSM maarufu kama wauza lambalamba AZAM FC imeibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya AFC kwa mabao yaliopachikwa wavuni na stadi wao na timu ya taifa Taifa Stars JOHN BOKO maarufu kama Adebayoo.

Huko Mwanza wana keshamapanda Toto Africans ya Mwanza ikatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba na kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabo mawili kwa bila dhidi timu iliyopanda daraja ya Ruvu Shooting kaka zao Ruvu JKT wao wakatoa kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya wenyeji wao KAGERA SUGAR mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

Wakati Mtibwa Sugar wakisafiri hadi mkoani Ruvuma waliibuka kidedea dhidi ya wenyeji wao Majimaji ya Songea kwa ushindi wa bao moja kwa bila, mchezo ulipingwa katika dimba la Majimaji mjini humo,ligi hiyo inasimama hadi septemba 11 kuipisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Algeria ugenini kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mchezo utakaopingwa nchini Algeria Septemba 4.

== =

No comments:

Post a Comment