Tuesday, August 31, 2010

Habari za michezo za kimataifa za leo

ALGERIA yaamini itafanya vizuri mchezo dhidi ya TAIFA STARS
WAKATI timu ya taifa, TAIFA STARS ikiwa njiani kuelekea ALGIERS kwaajili ya mchezo wa kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya ALGERIA, kocha wa timu ya taifa ya ALGERIA RABAH SAADANE amesema kufungwa na GABON katika mchezo wa kirafiki haimaanishi kuanza vibaya katika mchezo dhidi ya TAIFA STARS.
Kauli ya kocha huyo imeungwa mkono na beki wa kimataifa wa ALGERIA, MADJID BOUGHERRA ambaye naye anaamini kuwa kushindwa kwao nyumbani kwa magoli MAWILI kwa MOJA sio ishara ya kufungwa na STARS.
Miongoni mwa sababu alizozitaja zilizosababisha kufungwa na GABON ni kutokana na kwanza wachezaji wengi walikuwa hawana mazoezi na ni mwanzo wa msimu .
ALGERIA ambayo ilishiriki mashindano ya kombe la dunia ya mwaka huu nchini AFRIKA KUSINI inaanza kibarua chake kwa kucheza na TAIFA STARS mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON ya mwaka 2012.
==
FRANCISCO VARALLO afariki dunia
KATI ya wachezaji wachache wakongwe ambao walicheza katika mashindano ya kwanza ya kombe la dunia akiwemo FRANCISCO VARALLO wa ARGENTINA amefariki dunia akiwa na umri wa miaka MIA MOJA.
Picha ya VIDEO ya VARALLO ni kwa hisani ya mtandao kupitia YOU TUBE ambapo aliichezea timu yake ya taifa ya ARGENTINA katika mchezo wa fainali dhidi ya timu ya URUGUAY, mchezo uliochezwa URUGUAY mwaka 1930 na timu yake kufungwa magoli MANNE kwa MAWILI.
Wakati wa uchezaji wake VARALLO aliweza kuifungia timu yake ya BOCA JUNIORS magoli 194 rekodi ambayo imevunjwa mwaka huu na mshambuliaji wa timu hiyo MARTIN PALERMO.
Wakati wa mahojiano mwaka huu kabla ya kifo chake na FIFA , kuadhimisha miaka 100, VARALLO alisema anakumbuka vilivyo mchezo wa fainali wa mwaka 1930 na kubainisha kuwa ulimnyong`onyesha na hata kulia kwa kufungwa na URUGUAY.
VARALLO aliachana na masuala ya soka baada ya kuumia akiwa na umri wa miaka THELATHINI na kuanza kufanya kazi ya ukocha na timu za vijana za BOCA JUNIOR.
==
BOB BRADLEY asaini kuifundisha Marekani
KOCHA wa timu ya taifa ya MAREKANI, BOB BRADLEY amesaini makataba wa miaka MINNE kuendelea kuifundisha timu ya taifa ya MAREKANI kwa kipindi cha miaka MINNE ijayo.
Kutia saini kwa kocha huyo kunamaliza tetesi kuwa kocha huyo anakwenda kuifundisha timu ya ASTON VILLA.
BRADLEY ambaye aliipeleka MAREKANI raundi ya pili ya mashindano ya kombe la dunia ya Afrika kusini sasa atakaa katika timu hiyo hadi mwaka 2014.
BRADLEY alichukua jukumu la kuifundisha MAREKANI mwaka 2006 kutoka kwa BRUCE ARENA na BRADLEY ameisaidia MAREKANI kutoka sare na timu za ENGLAND na SLOVENIA kabla ya kuifunga ALGERIA goli MOJA kwa SIFURI na kuwa timu ya kwanza katika kundi lake la C na iliondolewa na GHANA kwa kuifungwa magoli MAWILI kwa MOJA.
==
Manyota wa TENNIS washinda raundi ya kwanza
Mchezaji ELENA BALTACHA amefanikiwa kuanza vizuri mashindano ya TENNIS ya wazi ya MAREKANI baada ya kumrarua PETRA MARTIC kwa seti 6-2 6-2 katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo.
BALTACHA, ambaye ni mchezaji bora wa 57 ulimwenguni anatarajia kupanda chati hiyo na kufikia namba 50.
Baada ya ushondi huo sasa BALTACHA atapambana na Kvitova baada ya KVITOVA naye kumfunga mwenzake LUCIE HRADECKA kwa seti 6-4 7-5.
Huku VENUS WILLIAMS naye akifanikiwa kumfunga ROBERTA VINCI kwa seti 6-4na 6-1.
Naye bingwa wa mara tano katika mashindano hayo ya MAREKANI upande wa wanaume ROGER FEDERER amefanikiwa kushinda mchezo wake wa awali kwa kumchakaza muajentina BRIAN DABUL kwa ushindi wa seti 6-1 6-4 6-2.
Ushindi wa FEDERER unamfanya sasa apambane na mjeruman, ANDREAS BECK katika raundi ya pili.
Wengine walioshinda michezo yao ni pamoja na MARIN CILIC na JUAN CARLOS FERRERO.
==
Timu za Afrika zafanya vibaya mashindano ya kikapu ya dunia.
Wawakilishi wa bara la Afrika katika mashindano ya dunia ya mchezo wa kikapu , TUNISIA na ALGERIA zimefanya vibaya katika michezo yao.
TUNISIA imefungwa na IRAN kwa vikapu 58 kwa 71, huku ARGERNTINA ikiigaragaza vikapu 91 kwa 70 timu ya Angola.
Huku BRAZIL ikichapwa na Marekani kwa vikapu 70 kwa 68, na AUSTRALIA ikirarua timu ya UJERUMAN kwa vikapu 78 kwa 43, CROATIA nayo ikachapwa na SLOVENIA kwa vikapu 91 kwa 84.
==

No comments:

Post a Comment