Wednesday, August 11, 2010

Marefa wanolewa

WAAMUZI wa soka hapa nchini kwa sasa wapo katika semina maalumu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara Agosti 21.
Mkufunzi mkuu na Mwenyekiti wa chama cha waamuzi nchini (FRAT) OMARY ABDULKADIR anasema baada ya mafunzo hayo wanategemea kupata waamuzi ambao watachezesha ligi katika kiwango cha juu japo wamegundua baadhi ya matatizo likiwemo tatizo la waamuzi kushindwa kutafsiri vyema sheria ya kuotea pamoja na kutoa adhabu inayokusudiwa kulingana na kosa.Waamuzi KUMI na SITA na wasaidizi wao THELATHINI na SITA watateuliwa kuchezesha ligi kuu TANZANIA BARA baada ya kufaulu mitihani yao ya majaribio yaani COPPER TEST

No comments:

Post a Comment