Thursday, August 26, 2010

Shirikisho la mpira wa miguu nchini limebadili kanunu zake za ligi na saa Ligi kuu Tanzaniza Bara itakuwa na timu kumi na nne badala ya 12 katika msimu wa 2011 /2012.
Afisa habari wa TFF Florian Kaijage amesema lego la mabadiliko hayo ya kanuni ya nne ya ligi kuu ni kuogeza ushindani kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo kwa lego la kukuza soka hapa nchini.
Kaijage amesema katika mabadiliko hayo timu nne zitapanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu huku timu mbili zikireka daraja.
Ligi kuu Tanzania bara kwa sasa imekuwa na timu 12 na timu mbili zimekuwa sikishuka daraja huku timu tatu zikipanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu.
==
Uwanja wa UHURU tayari umeanza kufanyiwa ukarabati baada ya kufungwa kwa muda wa miezi mitatu na kuzifanya timu za ligi kuu Tanzania Bara zilizokuwa zinatumia uwanja huo kutafuta viwanja vingine.
Akizungumza na TBC mfanyakazi mmojawapo katika uwanja huo TUGE SHEMU aliyataja maaeneo yanayofanyiwa ukarabati kuwa ni mifereji ya kupitishia maji kwenye sehemu ya kuchezea yaani (pitch).
SHEMU ameyataja maeneo mengine kuwa ni kujenga uzio upande wa mashariki mwa uwanja huo na eneo la geti la upende wa kazikazini,kuezua paa la jukwaa kuu na kuweka paa jingine pamoja na kufunga viti vipya na kupaka rangi.
Timu zilizoathirika na ukarabati wa uwanja wa UHURU ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara SIMBA,mabingwa wa Ngao ya Hisani YANGA,AZAM FC,AFRICAL LYON na RUVU JKT.
==

No comments:

Post a Comment