Wednesday, August 25, 2010


MKAZI anayeishi jijini DSM, DORAH TEMU amebahatika kuibuka mshindi wa kitita cha shilingi MILIONI MIA MOJA katika shindano la kubahatisha linaloendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi fedha hizo, afisa uhusiano wa kampuni ya TIGO, JACKON MMBANDO amesema katika shindano hilo la JIKOKI jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi MILIONI 338, zilitolewa na kati ya hizo mshindi DORAH TEMU alifanikiwa kuwashinda washiriki wengine kwa kuwa na pointi nyingi zaidi.

Mbali na zawadi hiyo, TEMU aliwahi kunyakuwa zawadi ya fedha MILIONI MBILI na MILIONI TANO.
==

No comments:

Post a Comment