Tuesday, August 31, 2010

Simba kulishitaki mwanasport


Kamati ya utendaji wa klabu ya Simba imetishia kulishitaki gazeti la michezo la Mwanasport kwa kuandika makala inayoukashifu uongozi wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM hii leo, mwenyekiti wa klabu hiyo ISMAIL ADEN RAGE amesema kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana imetoa siku kumi na nne kwa gazeti hilo kuomba radhi vinginevyo watalishitaki mahakamani na pia kudai kulipwa fidia ya shilingi bilioni moja kama litashindwa kufanya hivyo
Wakati huo huo Rage amesema klabu ya Simba itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ulizi ya Kenya siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini DSM ikiwa ni maadalizi ya kuikabili Azam FC katika mchezo utakaopingwa Septemba 11 katika uwanja wa taifa.
RAGE ameongeza kusema kwamba baada ya mchezo huo wachezaji wa samba watasafiri kwenda jijini mwanza ambapo watautumia uwanja wa CCM KIRUMBA kwa michezo yake ijayo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya uwanja wa Uhuru kufungwa kwa ajili ya mategenezo.
Simba imeanza vyema kuutetea ubingwa wake baada ya kuifunga African Lyon mabao mawili kwa bila katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Augosti 21.

No comments:

Post a Comment