Monday, August 23, 2010

STARS yaanza mazoezi kuivaa Algeria.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars kilichotangaza na kocha wake mkuu JAN POULSEN jijini Arusha hiyo jana kinaanza mozezi hii leo katika uwanja wa karume tayari kuikabili Algeria ungenini Septemba 4.

Katika kikosi kilichotangazwa jana hakina mabadiliko licha ya kocha huyo kushuhudia michezo miwili mikubwa,mchezo kati ya watani wa jadi Simba na Yanga uliopingwa siku ya jumatano kwania Ngao ya Hisani uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini DSM na ule wa uliopingwa katika uwanja wa Shekh Amr Abeid kati ya AFC na Azam FC.

POULSEN amerudisha kikosi kilekile kilichocheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars mchezo ulipingwa AUGOSTI 11 katika uwanja wa Taifa jijini DSM na timu hizo kufungana bao moja kwa moja ikiswa ni pamoja na mlinda mlango majeruhi JUMA KASEJA na kumuacha kiungo wa pembeni KIGI MAKASI.

Pia POULSEN amewateua katika timu yake wachezaji wanosukuma soka ya kulipwa Nizar Khalifan anayekipinga katika timu ya Vancouver White Caps ya Canada,Henry Josoph anayecheza Sweden, Danny Mrwanda anayecheza Veitnam na Idrisa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya.

Star itashuka dimbani kuikabili Algeria ugenini Septemba 4 kabla ya kuikabili MORROCCO Octoba 9 jijini DSM.

Stars imepangwa kundi moja na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Morocco na Algeria.

==

Ligi kuu ya Tanzania bara yasimama kuipisha Stars.

Ligi kuu Tanzania bara iliyoanza kutimua vumbi katika viwanja sita siku ya jumamosi imesimama hadi septemba 11 kuipisha Taifa Stars inayojianda kuteremka dimbani dhidi ya Algeria ugenini Septemba 3.

Katika michezo iliyochezwa juzi,Katika dimba la Uhuru mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Simba ukipenda waiti wekundu wa masimbazi wao waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya African Lyon.

Kwingineko mabingwa wa Ngao ya Hisani Yanga ilibuka kidedea baada ya kuichapa Polisi Tanzania kwa bao moja kwa bila.

Katika uwanja wa Shekh Amri Abeid jijini Arusha wanalambalamba AZAM FC iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya AFC.

Huko Mwanza wana kishamapanda Toto Africans ya Mwanza wakatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba na kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi timu iliyopanda daraja ya Ruvu Shooting.

Huko Kagera Ruvu JKT waliwachapa wenyeji wao KAGERA SUGAR bao moja kwa bila wakati Mtibwa Sugar waliifunga Majimaji ya Songea bao moja kwa bila,

== =

Mashindano ya ngumi ya Afrika ya Mashariki kuanza kesho

Mashindano ya ngumi za riadhaa ya Afrika ya Mashariki maarufu kama mabingwa wa mabingwa yanaanza kutimua vumbi hapo kesho jijini DSM huku mabondia wa Tanzania wakitamba kufanya vyema katika mashindano hayo.

Akizungumza na TBC kwa njia ya simu katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT) MAKORE MASHANGA amesema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika huku nchi zitakazo shiriki zikitazamiwa kuwasili jioni ya leo

Mashindano hayo yanashirikisha mabondia kutoka katika nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi ,Botwana na Morius na wenyeji Tanzania.

===

Mashindano ya UMISETA kwa timu za Afrika ya Mashariki yaanza nchini Kenya

Mashindano ya UMISETA kwa timu za Afrika Mashariki yameanza nchini Kenya huku timu za Tanzania zikianza kutupa karata zao za kwanza asubuhi ya leo.

Akiongea na TBC kwa njia ya simu mratibu wa UMISETA kwa timu za Tanzania SALUM SALUM amesema timu ya soka ya wasichana wa Tanzania imeteremka dimbani kuchuana na RWANDA.

SALUM amezitaja timu nyingine za Tanzania zitakazoshuka dimbani kuwa ni timu ya mpira wa kikapu itakayomenyana na Uganda, timu ya mpira wa wavu ya wasichana inaikabili timu ya SUDAN na timu ya mwisho kucheza itakuwa ni ya soka ya wanaume ya Tanzania itakayocheza na Kenya.

Mashindano hayo ya UMISETA ya Afrika Mashariki yanashirikisha timu kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda, Burundi na wenyeji Kenya,.

====

Liverpool uso kwa uso na Manchester city

Lgi kuu ya Uingereza itaendelea usiku wa leo kwa matajiri wapya wa ligi hiyo MANCHESTER CITY itakapowakatibisha majogoo wa jiji LIVERPOOL katika uwanja wa CITY OF MANCHESTER.

Kocha wa Liverpol ROY HOGSON anaamini vijana wake watacheza vizuri ugenini na kuibuka na ushndi katika mchezo huo huku kocha wa Man City ROBERTO MANSHINI akijigamba kuibuka kidedea katika uwanja wake wa nyumbani kwa usajili wa nguvu alioufanya msimu huu.

Katika michezo iliyochezwa jana Mashetani wekundu Manchester United walijikuta wakilazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya wenyehi wao FULHAM waliokua chini ya kocha wao mpya MARK HUGHES.

MANCHESTER ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lilofungwa na mgongwe PAUL SKOZI katika dakika ya 12 ya mchezo.

FULHAM wakaja juu katika kipindi cha pili na kusawazisha bao hilo kupita kwa DAVIS lakini MAN UNITED wakajipatia bao la pili baada ya beki wa FULHAM BREDE HANGALEND kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona

LUIS NANI akaikosesha MAN UNITED bao la tatu na pengine lingekua la ushindi lakini penati yake aliyopinga zikiwa zimesalia dakika sita mpira kumalizika ikaenda mikononi mwa kipa wa FULHAM, DAVID STOCKDALE.

Fulham wakafanya shambulizi la mwisho na kupata kona ambayo ilizaa bao lilofungwa na beki wake BREDE HANGALEND.

Katika mchezo mwingine ulichezwa jana ASTON VILLA ilipata kichapo cha mabao sita kwa bila kutoka kwa timu ya NEW CASTLE UNITED

== =

Federer Bibgwa wa Western and Southern Masters

ROGER FEDERER ameshinda taji lake kubwa la 17 la tenisi baada ya kumchapa Mmarekani MARDY FISH kwa ushindi wa seti 2-1 ya 6-7,7-6 na 6-4 katika mchezo wa fainali iliyokua ya kusisimua ya WESTERN AND SOUTHERN FINANCIL GROUP MASTERS iliyofanyika jana nchini MAREKANI.

FEDERER mchezaji nambari mbili kwa ubora wa tenisi duniani ilibidi afanye kazi ya ziada kumdhiibiti mpinzani wake FISH baada ya kufungwa katika seti ya kwanza kwa 7-6.

FEDERER alikuja juu na kucheza kwa ustadi mkubwa na kushinda katika seti ya pili na ya tatu baada ya kupata shindi kwa seti 7-6 na 6-4.

Hili ni taji la NNE la WESTERN AND SOUTHERN FINANCIL GROUP MASTERS kwa FEDERER na likiwa ni taji lake la 17 la mashindano makubwa akiwa nyuma ya Mmarekani ENDRE AGASS mwenye mataji 18.

===

No comments:

Post a Comment